Tuesday, April 18, 2006

UTANDAWAZI NA ATHARI ZAKE KWA AFRIKA

Katika dunia ya leo neno utandawazi limetawala maisha ya kila siku na kumekuwepo mjadala juu ya faida na hasara zake hususan kwa mataifa maskini.

Utandawazi kimsingi unaweza kuelezwa kuwa ni mchakato wa kuunganisha uchumi,siasa,jamii,uhusiano wa tamaduni n.k baina ya nchi, utandawazi unaifanya dunia kuwa kama kijiji kimoja kisicho kuwa na mpaka! Utandawazi unasisitiza uondoaji wa vikwazo vya kibiashara na kuifanya dunia kuwa soko moja,unahimiza soko huria,demokrasia,utawala bora,usawa wa kijinsia, haki za binadamu, utunzaji wa mazingira n.k miongoni mwa jamii husika.

Utandawazi siyo dhana mpya kama inavyotaka kuaminishwa na baadhi ya wasomi mbali mbali hapa duniani.tukiangalia historia inaonyesha kuwa utandawazi ulianza zamani sana enzi zile za Christopher Clombus alipokwenda Amerika na kuingiza mazao ya miwa,machungwa na uchimbaji mkubwa wa madini.

Afrika iliingizwa katika utandawazi rasmi enzi za biashara ya utumwa iliyojulikana kama “The Trans –Atlantic Slave Trade” Afrika ilifanywa kuwa chanzo cha nguvu kazi ya bei rahisi, ambapo watumwa walipelekwa bara la Amerika katika mashamba na migodi mikubwa, baada ya mapinduzi ya viwanda biashara ya utumwa ilionekana kutokuwa tena na faida na hivyo ilisitishwa.

Wa Afrika walionekana kuwa wanaweza kuzarisha malighafi kwa ajili ya viwanda vya Ulaya na pia kuwa soko kwa bidhaa za viwandani kwahiyo mnamo mwaka 1884 ulifanyika makutano huko Ujerumani, maaarufu kwa jina Mkutano wa Berln, mkutano huu ulikuwa mahususi kuligawa bara la Afrika kwa watawala mbali mbali, makoloni yalihimizwa kuzarisha malighafi kwa ajili ya viwanda vya Ulaya, kwa mfano makoloni yaliyokuwa chini ya Muingereza yalizarisha kwa ajili ya nchi hiyo.

Baada ya hapo kiliingia kipindi cha miaka ya 1960s ambapo mataifa mengi ya bara la Afrika yalipata uhuru wake hususan uhuru wa siasa, kwani kiuchumi hali iliendelea kuwa ya utegemezi.

Katika muongo huu tumeshuhudia nene jipya ambalo ni utandawazi, makala hii inajaribu kuangalia ahtari ambazo Afika imekumbana nazo na hususan kiuchumi.

Kwanza umasikini katika bara la Afrika ni asilimia 40 mpaka 50, wananchi wake wanaendelea kuishi katika hali ya umaskini kwa sababu ya ukosefu wa kipato kwa kaya na kibaya zaidi nguvu kazi inaendelea kukua kwa kasi ya asilimia 4 mpaka tano kwa mwaka na hakuna juhudi muhususi za kuitumia nguvu kazi hiyo katika uzarishaji na kazi za maendeleo.

Pili Afrika inapokea asilimia 1 ya vitega uchumi toka nje(fdi) na vingi kati ya hivyo vimekuwa vinalundikana katika baadhi ya nchi za Kaskazini,nchi zinazo zalisha mafuta na Afrika Kusini na kuziacha nchi nyingine zikiambulia vitega uchumi vichache sana na hivyo kushindwa kufaidika na uwekezaji ambao umeongezeka duniani hivi leo kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo dunia inayo hivi sasa.

Tatu bara la Afrika ni mshiriki duni katika uchumi wa dunia,pato lake ni sawa na asilimia 1 ya uchumi wa dunia(GDP), uchumi wa Afrika nzima unauzidi kidogo uchumi wan nchi ua Ubeljiji,ikilinganishwa na Ubeljiji ambayo amabayo ni nchi ndogo sana hata kwa kuilinganisha na Tanzania

Nne utandawazi unahimiza biashara huria baina ya mataifa bila kuzingatia nani anashindana na nani na wanashindania nini?kwa mjibu wa Christian Aid inakadiriwa kuwa biashara huria imesababisha uharibifu kwa bara hili kiasi cha dola za kimarekani bilioni 272 kuanzia mwaka 1980

Tano nchi za dunia ya tatu zinatumia kiasi cha dola za kimarekani 340 bilioni kulipa madeni yanayokadiriwa kufikia dola 2,2 trilioni, kiasi ambacho ni mara tano zaidi ya bajeti ya nchi za G8 inayotolewa kwa nchi hizo kama misaada ya kimaendeleoi!

Sita pengo kati ya nchi tajiri na maskini linazidi kuongezeka, kwa mfano miaka 20 iliyopita wastani wa uwiano wa kipato kati ya nchi maskini sana duniani(LDCs) na nchi tajiri ulikuwa 1:87 kwa hivi sasa unakadiriwa kuwa1:98, maana yake ni kuwa utandawazi unazidi kuzinufaisha zaidi nchi tajiri na makampuni ya kimataifa kulikoni nchi maskini na makampuni yake

Dunia ya utandawazi haina huruma na umaskini na isitarajiwe kabisa kuwa nchi tajiri na makampuni yake yana dhati ya kweli kuondoa umaskini huo,je zifanye hivyo kwa faida ya nani?

Saba kilimo ni uti wa mgongo wa nchi nyingi za bara la Afrika, inakadiriwa kuwa asilimia 70 ya watu wa bara hili wanategemea kilimo,pia kilimo kinachangia katika pato la taifa asilimia 30(30%of GDP), ni jambo la kusikitisha kuwa ni Afirka pekee ambapo tija katika kilimo haijaongezeka kwa muda wa miaka 20 yaani kuazia mwaka 1980 mpaka 2000

Bara la Afrika miaka 50 iliyopita liliweza kujitosheleza kwa chakula na ziada kuuza nje, inasikitisha kuona kuwa hivi sasa Afrika inaongoza kwa kuagiza chakula toka nje ya bara la Afrika, kwa mfano mwaka 1966 mpaka 1970 Afrika iliuza nje wastani wa tani 1.3 milioni za chakula kwa mwaka, na mwisho wa miaka 1970s Afrika iliagiza tani 4,4 milioni za chakula kwa mwaka na takwimu zinaongezeka kufikia tani 10 milioni kwa mwaka mpaka ilipofikia mwaka 1980

Nane katika dunia ya leo bado Afika watu wanaokadiriwa kufikia milioni 200 hawana chakula, na inakisiwa kuwa nchi 27 za kusini mwa Afrika zinahitaji msaada ya chakula,bara lililo kuwa linauza chakula nje hivi sasa linahitaji msaada, tena wakati huu ambapo kuna mapinduzi katika uzarishaji wa kilimo kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Kwa mjibu wa shirika moja la Uingereza la Oxfam inakadiriwa kuwa nchi tajiri zinatumia kiasi cha dola bilioni moja kwa siku kwa aili ya kutoa rudhuku kwa wakulima wa nchi hizo,kiashi hicho ni sawa na pato la nchi maskini sana duniani(LDCs), katika dunia ya namna hii itawezekana vipi mkulima katika Afrika kuweza kushindana na mkulima kutoka nchi tajiri katika soko la kimataifa?

Tisa kiasi cha madini kilichoko ardhini kinapungua kila kukicha, nchini Afrika Kusini mwaka 1960 kulikuwa na na madini yenye thamani ya dola 112bilioni na mwaka 2000 inakadiriwa kuwepo madini yenye thamani 55bilioni hii ni kutokana na ripoti za UN,kwa ujumla Afrika inapoteza sana kuliko inavyopata katika madini.

Kumi mwaka 2004 Alpha Oumer Konare aliukumbusha mkutano wa Afrika kuwa bara la Afrika katika kipindi cha miaka 50 limeshuhudia jumla ya mapinduzi ya serikali yapatayo 186,vita kubwa 26 na wakimbizi wapatao milioni 16 , matatizo yote hayo ukiyaangalia kwa makini yana mkono kotoka nchi za nje ya bara la Afrika kwa njia moja au nyingine.

Kumi na moja uwiano wa mapato duniani ni wa kutisha sana , kwa mjibu wa ripoti iliyotolewa na UNHD(Nationas Human Development) watu 1.3 bilioni wanaishi chini ya dola moja kwa siku wakati huo huo watu 200 ambao ni matajri sana duniani waliweza kuongeza utajiri wao kati ya mwaka1994 mpaka 1998 na inakadiriwa kuwa utajiri wao unao zidi dola 1 trilioni, si hivyo tu kwani mabilionea watatu wanao ongoza kwa utajri duniani wanamiliki mali zenye thamani kubwa kuliko mapato(GNP) ya nchi zile maskini sana duniani (LDCs) zikiwa na watu milioni 600!

Kumi na mbili tofauti ya mapato (income gap) kati ya nchi tano kwa wingi wa watu duniani katika nchi tajiri na ya tano kwa wingi wa watu duniani katika nchi maskini ilikuwa 74:1 mwaka 1997,60:1 mwaka1990 na 30:1 mwaka 1960,wale wanao ishi katika nchi tajiri duniani wanamilki pato la dunia(GDP) kwa asilimia 86,wanamilki asilimia 82 ya mauzo ya nje,asilimia 68 ya vitefa uchumi toka nje(FDI) asilimia74 ya njia za simu za dunia(world telephone lines) n.k wale wanaoishi katika nchi maskini sana duniani wana ambulia asilimia 1 tu ya yaliyo tajwa hapo juu, Pia nchi hizo tajiri zikiwa na asilimia 19 ya idadi ya watu wote duniani zinamilki biashara ya dunia kwa asilimia 71!

Ukiangalia nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara kwa ujumla wake asilimia 50 ya watoto wake hawana huduma ya maji salama,moja ya tatu ya watoto wenye umri wa miaka 5 wana uzito pungufu(underweight) na zaidi ya robo tatu ya watu wake hawatarajii kuishi zaidi ya mika 40 wakati ulaya ni zaidi ya miaka 70

Utajiri wa dunia umo mikononi mwa wachache kwa mfano mpaka kufikia mwaka 1998 makampuni kumi tu ya madawa ya kilimo yalimilki asilimia 85 ya dola 31 bilioni ya soko la dunia, makampuni makubwa kumi duniani ya mawasiliano yanamilki asilimia 86 ya dola 262bilioni ya soko la dunia,katika biashara ya komputa makampuni kumi makubwa duniani yanamilki asilimia 70 ya soko la komputa duniani,asilimia 60 ya madawa ya mifungo yapo chini ya milki ya makampuni kumi makubwa duniani.

Kutokana na mlundikano wa namna hiyo nchi maskini duniani zinapata faida haba inayotokana na maendeleo ya sayandi na teknolojia na elimu kwa ujumla, kwa mfano nchi kumi zinamilki utafiti na matumizi ya maendeleo duniani na zinamilki asilimia 95 haki miliki ya marekani(patent), kwa sababu hiyo utafiti unazingatia sana faida na siyo mahitaji ya kijamii,katika kuteua dondoo za utafiti pesa ndiyo inayo ongea na siyo mahitaji, ndio maana tafiti za madawa ya vipodozi na nyanya zinazoiva kidogo kidogo zinapewa kipaumbele kuliko tafiti za mazao yanayositahimili ukame au kinga ya malaria.

Uchumi mkubwa duniani 100 , makampuni ni51 na nchi ni 49, Afrika ikiwa na nchi tatu tu ambazo ni Afrika kusini nafasi ya 34, Misri nafasi 88 na Algeria nafasi ya 89,kampuni ya Mitsubishi ni ya 22 ikizizidi inchi zipatazo 169 kwa kuchukua kumbukumbu kuwa duniani kuna nchi 191,M,Marubeni ni ya 28 n.k hii ni kwa mjibu wa ripoti za mwaka1995 hata kama kuna mabadiliko yatakuwa si makubwa sana.

Kumi na tatu dunia ya leo ya utandawazi inahitaji watu walioelimika ambao wataweza kutumia fursa za utandawazi kama zipo,Afrika inaendelea kuwa nyuma katika kuwekeza katika elimu,kiwango cha ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika ni asilimia 41.

Hii ndiyo dunia ya leo ambayo Afrika inahimizwa sana kishiriki,dunia ambayo inathamini mwenye nguvu ya mtaji,IMF , Benki ya dunia na Shirika la Baishara Duniani(WTO) ndio wadau wakuu wa utetezi wa biashara huria inayotawaliwa na nguvu za soko,mkulima maskini toka Tanzania anaambiwa ashindane katika soko la kimataifa, na mkulima wa Ulaya au Marekani anayepatiwa rudhuku “super market kama vile IMALASEKO ya hapa Tanzania inaambiwa ishindane na Wal-Mart(kampuni ya kimarekani inayoshika nafasi ya 48 duniani),kampuni ya magari ya Nyumbu inaambiwa ishindane na Mitsubishi(inayoshika nafasi ya 22),kampuni ya posta Tanzania ianaambiwa ishindane na AT&T (inayoshika nafasi ya 48) n.k ,katika hali halisi haiwezekani kabisa,serikali za nchi za Afrika zinapaswa kuuangalia utandawazi kwa mapana yeke,utandawazi wa kuzidi kuziimarisha nchi tajiri na makampuni yake na kulifanya bara la Afrika kuzidi kuwa maskini haupaswi kukumbatiwa kabisa, hakuna wa kuliangalia bara la Afrika kwa jicho la huruma ni juu ya viongozi wetu kuwa na visheni na kuona ni kwa jinsi gani tutakuwa na mfumo wa maisha ambao wadau wote watanufaika nao,ukubwa wa uchumi wan chi za magharibu namakampuni yao usitukatishe tama wala kutuogopesha kuwa hatuwezi,kwani kama kizazi kilichotangulia kingeogopa nguvu za kijeshi za wakolini hakuna nchi ambayo ingekuwa huru hivi leo,kizazi cha uhuru wa kisiasa kilifanya kazi yao hivi leo tunahitaji uhuru wa kiuchuimi na ni jukumu letu sote kupigana vita ya kujikoboa kiuchumi na kuondokana na umaskini tulio nao katika bara la Afrika,hakuna lisoliowezekana, kupanga ni kuchagua
Makala hii ilitoka katika gazeti la Tanzania daima

innokahwa@yahoo.com.tel 0744292718

Sunday, April 16, 2006

KAMPENI NI NJIA YA KUWASILIANA NA WAPIGA KURA

Kwa takribani yapata miezi mitatu tangu kampeni za uchaguzi wa madiwani,ubunge na urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania zianze na hatima yake ni mwezi huu tarehe14 ambayo ni siku ya kupiga kura.

Kimsingi wanasiasa kipindi chote hicho wamekuwa katika soko tena soko huria wakijaribu kunadi sera, katika soko kinachonadiwa ni bidhaa(product) yaani kitu chochote kinachoweza kutolewa na kuridhisha hitaji la mtu, na ieleweke kuwa katika kampeni kinachokuwa kinauzwa ni sera na mzarishaji(producer/manufacturer) ni vyama, na tukiangalia katika soko letu hili kulikuwa na wazarishaji mbali mbali kuanzia wadogo mpaka wakubwa, kama ilivyo katika biashara za kawaida ambapo kuna makampuni makubwa mfano katka soko la vinywaji baridi kuna kampuni inauza coca cola,pepsi cola,super cola n.k vivyo hivyo katika soko la siasa kulikuwa na vyama kadha wakadha kama vile CCM,CUF,CHADEMA,TLP,NCCR-mageuzi,CHAUSTA,UDP n.k

Ukubwa wa kampuni yeyote unategemea na vigezo unavyotumia, unaweza kutumia asilimia ya umilikaji wa soko(%market share),mauzo(sales) n.k sawia katika ukubwa wa chama unaweza kuangaliwa kwa kutumia vigezo tofauti kama vile idadi ya wanachama,idadi ya wabunge na madiwani,mtandao wa chama, idadi ya washabeki na wapenzi n.k

Katika soko la bidhaa za kawaida kama vile soda,magari,simu,hotel,benki,muziki n.k umuhimu mkubwa hawekwi kwenye bidhaa(product) bali uzingatiaji mkubwa uwekwa kwa mtumiaji/mnunuzi(consumer/customer),afisa masoko mzuri ataweka kipaumbele zaidi katika hitaji la mteja kuliko bidhaa, kwani bidhaa utumika kama behewa(vehicle) la kutatua shida ya mteja.Hivyo ni vyema na busara sana ukajua mteja anataka nini? alafu ndiyo ukatengeneza bidhaa ya kuweza kutatua tatizo lake, vivyo ilivyo katika siasa ni vyema chama kikaanza kujiuliza mwananchi anashida gani? Kutokana na shida au tatizo husika ndipo sera uandaliwa kukidhi shida inayomkabili mwananchi, chama kisicho zingatia hayo kitegemee muujiza zaidi kupata kura za mwananchi labda katika soko la walaji wasiojua wanataka nini?.

Haitoshi tu kuwa na bidhaa nzuri kiwandani au dukani pasipo kuwasiliana na wateja au walaji(communicate the value to customers) ndiyo maana vyama vyote vya siasa baada ya kuwa vimejua shida na kero za wananchi vilikaa chini na kuandaa sera zenye kutoa majibu ya matatizo ya wananchi , sera kama vile za elimu,afya, kilimo,ufugaji,madini ,maji, ajira n.k chama chochote kitakuwa kimefanya kosa kubwa sana kwa kuandaa sera na kukaa nazo tu ofisini pasipo kuwasiliana na wananchi.

Katika siasa za ushindani kuna njia nyingi zinazoweza kutumika kujitangaza, lakini kabla hujaamua ni njia ipi itumike ni vyema mambo yafuatayo yakazingatiwa

Kwanza adhila iliyokusudiwa, akina nani? ni vijana, wazee,wanawake, wanaume,wakulima, wafanyakazi,wavuvi n.k ni muhimu sana kuijua adhila katika kampeni mara nyingi wapiga kura katika nchi maskini ni vijana na watu wa rika ya kati na wanawake, wazee sana ni wachache pamoja na hayo haipaswi wazee kudharauliwa na kuachwa maana katika uchaguzi kura moja ina thamani kubwa katika kuamua mshindi, mgombea aliyefanyikiwa kujua adhila anayowasiliana nayo anakuwa na nafasi kubwa sana kufikisha ujumbe uliokusudiwa, katika mawasiliano kuna hatua zifuatazo kwanza mtumaji (sender) pili ujumbe(massege) tatu njia(means) na nne mpokeaji(receiver) na mwisho ni mshindo nyuma (feedback) ni vyema ujumbe ukafika na ukaelewaka la sivyo itakuwa ni kazi bure na ndiyo maana baadhi ya wagombea baada ya kugundua kuwa adhila ni vijana wasikuwa na kazi lugha au maneno kama haya yalisikika yakutumika’’ washikaji’’ ,‘’mmepigika’’, ‘’hakuna kulala mpaka kieleweke’’ nk hii yote ni njia ya kutengeneza ujumbe utakao eleweka na adhila husika.

Si hivyo tu, bali habari gani wanataka ? ni vyema mgombea akajua kuwa pamoja na kuwa kila chama kina ilani ambayo ni mjumuisho wa sera zote kwa ujumla wake adhila yake inataka kusikia nini? kwa mfano mgombea anayewasiliana na wapiga kura walioko machimboni Mwadui,Geita,Melelani n.wangependa sna kusikia zaidi sera inayohusu madini ,itakuwa ni kupoteza muda na fedha bure kuwaeleza habari za uvuvi au kilimo n.k.

Chombo gani kitumike? Mgombea ni vizuri akajua wapiga kura wake wanapendelea zaidi chombo gani cha mawasilino kama ni Radio na mgombea yupo Dar es salaam ni vyema akafikiria Radio za FM na pia ni lazima ajue ni fm gani? Kama ni tv ni tv gani ? kama gazeti ni gazeti gani? n.k

Pili mgombea sharti akajua lengo na dhumuni la kuwasilina ni nini? je ni kujitambulisha( creating awareness) ,kushawishi (convince), kukubusha(remind) au ni vyote kwa pamoja maana katika kampeni mgombea anaweza akawa ndiyo kwanza anajitambulisha pia akawa anajaribu kushawishi ili yeye aonekane ndiye bora na hivyo achaguliwe yeye pia inaweza ikiwa anawakumbushia tu kuwa yeye ndiye mgombea bora, katika mazingira ya namna hioyo ni vyema mgombea akaonyesha ni kwanini achaguliwe yeye na si mshindani wake na hivyo haiepukiki kutomuongelea mshindani wako ili yeye aonekani hafai akilinganishwa na wewe, na wewe ndiye unafaa kuwa diwani,mbunge au rais hapa swala siyo kukashifiana na kuzushiana mambo ya ovyo bali kuongelea sifa zako za msingi ukizilinganisha na za mshindani wako,ni vyema mgombea akajenga uhaminifu(loyalty) kwa wapiga kura ili ata akija mshindani wake haseweze kuwageuza wapiga kura wake na hivyo siku ya kupiga kura tarehe 14 mwezi huu wampigie yeye, ukiwa na wapiga kura "wasiyokuwaroyal" kwako basi ujue bado haujafanyikiwa kuwanasa.

Tatu katika kampeni kuna njia nyingi za kuweza kuwasilina na wapiga kura yaweza kuwa ni tangazo katika gazeti ,radio,tv ambapo ujumbe fulani mfano ‘’…kwa maendeleo ya taifa lako mchague x’’ pia mahusiano(publicity and public relations) ni muhimu sana kwa chama na mgombea yeyote aliyedhamiria kushinda katika uchaguzi wa tarehe14 mwezi huu, njia hii utumika kujega na kuimarisha jina zuri la chama au mgombea na kuzika habari mbaya za chama au mgombea mfano endapo itatokea chama Y kikahusishwa na habari mbaya ni vyema juhudi zikafanyika kujenga jina zuri la chama au mgomnbea katika kipindi hiki cha uchaguzi vyama na wagombea mbali mbali vimeonekana kufanya hivyo katika kipindi hiki cha uchaguzi na ni jambo zuri na kupongezwa kwani inaonyesha ni kwa jisi gani walivyo makini na kuendesha mambo kitaalamu. Pia mabango,kofia,t-shirt,khanga,vipeperushi hizo zote ni njia za kujitangaza kwa wapiga kura na ni kweli kuwa vitu hivyo vinahitaji pesa nyingi sana na hivyo ni vyema vyama vikawa vinajiandaa kwa hilo, uchaguzi hapa Tanzania ufanyika kila baada ya miaka mitano ni muda wa kutosha kwa chama makini kuweza kuwa na mpango wa kutenga bajeti kidogo kidogo kila mwaka na inapofika mwaka wa uchaguzi tayari chama kinakuwa na pesa kwa ajili hiyo, tatizo lililopo kwa vyama vingi ni kuendesha mambo kwa mpango wa zima moto,uchaguzi siyo jambo la kushutukizwa ni jambo linalo julikana kabla ya miaka mitano,

Vyama kukaa na kulalamika kuwa havina fedha za kampeni si la msingi sana bali jitihada zifanyike mapema kutafuta pesa na wakati mwingine ni swala la uvivu wa kufikiri na kutokuwa wabunifu tu, ni nani aliyejua au kutarajia kuwa chama fulani kingiweza kutumia helikoputa, kwa mwaka huu helikoputa inachukua nafasi zaidi ya usafiri ni ‘’promotional material’’inamtangaza mgombea na chama husika ina kijenga chama kwa wapiga kura huu ni ubunifu wa chama badala ya kutumia vitu ambavyo ni ‘’traditional’’ chama kinakuja na kitu kipya kwa mazingira ya uchaguzi wa Tanzania na 2010 helikoputa inaweza isiwe kivutio kama mwaka huu hiyo ndiyo chamgamoto ya kusoma wakati na mazingira na kuyatawala. Mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine.

Kama ilivyo biashara huria ilivyo jaa ushindani mkubwa sana vivyo hivyo siasa ya vyama vingi ina ushindani mkubwa sana, zama za kukaa maofisini na kuandaa sera pasipokujua ni nini matatizo ya wananchi zimekwisha,zama zakuleta wagombea bila kujali wapiga kura wanataka kiongozi wa aina gani ili waweze kushirikiana naye kuleta maendeleo hazipo tena,wakati wa bidhaa mbovu na hafifu sokoni haupo tena wakati wa sasa ni wa mzarishaji kwanza kujua hitaji la mteja na kutengeneza bidhaa inayokidhi hitaji na kuwasiliana na mteja ukimjulisha kuwa bidhaa safi na bora iko sokoni.

Wakati umebadilika na unazidi kubalika tena kwa kasi ya ajabu sana siasa ya leo si ya jana na siasa ya kesho si ya leo,inahitajika viongozi wasiyosubiri mabadiliko yawabadilishe wao bali viongozi wanaoleta mabadiloko na kuyasimamia mabadiliko hayo,

Mengi yamesemwa, mengi yameandikwa,ahadi nyingi zimetolewa , kilikuwa ni kipindi cha wagombea na vyama vyao kusema na kusikilizwa sasa ni zamu ya wapiga kura kusema kuwa tumewasikia na kuwaelewa na hiyo itafanyika kupita kura yako wewe mwanachi uliyejiandikisha , ni wakati wako kusema kilicho ndani ya mwoyo wako na wala usishinikizwe na ahadi ya uhongo,takrima,rushwa,ukabila,udini we sema tu siku hiyo ya tarehe14 mwezi huu na tume ya taifa ya uchaguzi itatangaza kwa sauti kubwa nini ulichokisema kwa kweka alama ya NDIYO kwa chaguo lako la diwani,mbunge na rais

Makala hii ilitoka katika gazeti la Tanzania daima mwaka jana kabla ya Uchaguzi MkuuMUANDISHI NI MSOMAJI NA MMFUATILIAJE WA SIASA ZA NDANI NA NJE YA TANZANIA

MWISHO

MKUU WA JESHI LA POLISI ANAPOTOA TUHUMA KWA MSINGI WA HISIA!

Nchini Tanzania tumezoea kuwasikia wanasiasa wakitoa tuhuma mbali mbali juu ya wapinzani wao wa kisiasa pasipokuwa na ushahidi wowote na wanapobanwa ujitetea kuwa hizo zilikuwa ni kauri za kisiasa kana kwamba wanasiasa wameruhusiwa kufanya hivyo! Tabia hii ya kutoa tuhuma nzito imeonekana kuwa ni mtindo kwa watanzania wengi na inaonekana rais mstaafu W. Mkapa hakupendezwa kabisa na mtu yeyote kumtuhumu mwenzake pasipo kuwa na ushahidi na mara kwa mara alikemea swala hilo na alisisitiza umuhimu wa tuhuma kuambatana na ushahidi.


Ukiangalia majukumu ya jeshi la polisi kwanza ni kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za zinalindwa (maintain law and order), ni jukumu la jeshi la polisi kuhakikisha kuwa sheria zilizo tungwa na bunge letu zinatekelezwa na wananchi wote pasipo kubagua mtu yeyote,jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine na wananchi kwa ujumla ujitahidi sana kuhakikisha kuwa sheria na taratibu zinafuatwa kwa faida ya watu wote na hivyo kuifanya nchi kuwa mahali salama pa kuishi na kufanya shughuli mbali mbali za maendeleo ya taifa letu.

Pili Jeshi la polisi limekasimiwa majukumu ya kulinda maisha ya raia na mali zao(protection of life and property) hivyo ni jukumu la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine kuhakikisha maisha na mali za wananchi wa Tanzania ziko salama , hivyo ni jukumu la polisi kuhakikisha kuwa vitendo vya ujambazi ambavyo vinaonekana kuongezeka kwa kasi hivi karibuni na kusababisha mali na maisha ya watanzania kuwa hatarini vinapunguwa kama si kuondolewa kabisa.

Tatu ni kugudua vitendo vya uhalifu (detection of crime), kukamata(arrest),kuedesha mashitaka, usalama barabarani,kulinda sera za nchi (safeguard the policy of the country) na ni jeshi la akiba, hayo ndiyo majukumu ya jeshi la polisi kimsingi,

Kwa nujibu wa sheria jeshi la polisi halipaswi kwa njia yoyote kushabikia au kuwa mpenzi wa chama fulani cha siasa, pia polisi wakiwa kama watumishi wa chombo cha dola hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa.


Makala hii ni matokeo ya matamshi ya mkuu wa jeshi la polisi afande Omary Mahita kama alivyo kaririwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa Chama cha CUF kinahusika na vitendo vya ujambazi hapa nchini! pia kuwa yeye akiwa mkuu wa jeshi la polisi chama cha CUF akitaingia madarakani mpaka kiama!

Baada ya kusoma magazeti kadha na kumsikia katika televisheni nimejiuliza maswali kadha na kuamua kuandika makala hii.

Kwanza nani kampa madaraka Mahita ya kuchagua chama cha kuingia madarakani?kutokana na sheria ya uchaguzi ,rais ,wabunge na madiwani uchaguliwa na wananchi wa Tanzania kwa kupigiwa kura ya siri,na ni Tume ya Uchaguzi ya Taifa yenye mamlaka ya kumtangaza mtu kuwa rais,mbunge na diwani sasa Mahita nguvu za kusema kuwa chama cha CUF hakitaingia madarakani mpaka kiama anazitoa wap?, kwani kwa kuangalia majukumu ya jeshi la polisi kama nilivyoyataja hapo juu hakuna kifungu kunachompa mamlaka hayo, pia ukisoma sheria ya uchaguzi hakuna kifungu kinacho mpa madaraka hayo ,sasa ni jambo la kushangaza kumsikia kiongozi mkubwa wa jeshi la polisi kama yeye akitoa maneno kama hayo, pia kwa mujibu wa sheria ya usajiri wa vyama vya siasa, chama usajiriwa na msajiri wa vyama vya siasa baada ya kukidhi matakwa ya sheria ya vyama, na chama chochote kilichosajirwa kinayo haki kisheria kushiriki katika uchaguzi na kuomba ridhaa ya kuongoza nchi toka kwa wapiga kura na si kwa afande Mahita..

Kuongezeka kwa vitendo vya ujambazi kwa siku za karibuni kusiwe chanzo cha kuleta vurugu nchini, viongozi bado wanapaswa kutambua kuwa nchi bado inaendelea kutawaliwa kwa kufuata katiba na sheria mbali mbali za nchi hii.

Katika sheria za nchi sidhani kama kuna kifungu kinachomuhalalisha mkuu wa jeshi la polisi kukituhumu chama au mtu yeyote kwa kutumia hisia! Mahita amekaririwa akisema kuwa anahisi kuwa vitendo vya ujambazi vinavyofanyika hivi sasa ni hujuma inayoandaliwa na chama cha CUF! Hapo ndipo ninapo pata tatizo kumuelewa afande wa jeshi la polisi.

Kwanza yeye hakupaswa kulalamika na kuutangazia umma wa watanzania juu ya hisia zake, kwani kwa mujibu wa uchunguzi kama taaluma agezifanyia kazi kwanza hisia zake kwa kuamru upelelezi kufanyika ili kukusanya ushahidi wa hisia zake na baada ya kujiridhisha na ushahidi alioukusanya angewakamata na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa na siyo kukimbilia kwenye vyombo vya habari,tatizo la Mahita anakuwa mwanasiasa zaidi kwani ni tabia ya wanasiasa wengi ulimwenguni kupenda kuonekana katika vyombo vya habari pasipo kuwa na sababu za msingi, tangu lini jeshi la polisi likawa linatangaza hisia za mtu na kuwambia watuhumiwa kuwa najiandaa kuja kuwapekuwa! Hivi hata kama ingekuwa kweli viongozi wa CUF kuwa wanashirikiana na majambazi, je taaluma ya upelelezi inamtaka Mahita awatangazie kwenye vyombo vya habari kabla ya kuwapekuwa na kuwakamata? Hii si ndiyo kuwapa nafasi ya kuficha silaha na ushahidi mwengine ambao ungekuwa muhimu kuthibitisha tuhuma?

Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana Disemba Mkuu wa jeshi la polisi alikaririwa na vyombo vya habari akikituhumu chama cha CUF kuwa kilishiriki kuingiza visu vyenye rangi na nembo zinazotumika na chama hicho lakini ni jambo la kushangaza kuwa hatujasikia mpaka hivi sasa ni watuhumiwa wangapi wamefikishwa mahakamani kwa kuingiza nchini visu kama hivyo,je watengezaji wa visu hivyo wamehojiwa na kukiri kuwa visu hivyo viliagizwa na CUF,je vililipiwa ushuru bandarini,uwanja wa ndege au mpakani? Je maofisa forodha waliovikagua visu hivyo wamehojiwa, Je unatofautishaje swala la chama na mwanachama au mpenzi binafsi? n.k hayo ndiyo mambo ya msingi ambayo Mahita angetakiwa kuyafanyia kazi kabla ya kukimbilia katika vyombo vya habari,

Inapotokea mkuu wa jeshi la polisi anaendesha jeshi kupitia katika vyombo vya habari hapo ndipo uwezo na mbinu za mkuu huyu vinapotia shaka sana, kufoka na kutumia lugha kari si mbinu wala mkakati muhususi wa kupambana na uhalifu nchini, hizo ni mbinu za mwaka 1940s, dunia ya sasa haitaji makeke bali ni mbinu za kisayansi zaidi na pengine ukimya zaidi unaonekana kufanya kazi, wananchi wanapenda kusikia watuhumiwa wakiwa wamefikishwa mahakamani na ushahidi.


Vitendo vya ujambazi vinavyofanyika hapa nchini vanatumia bunduki na siyo visu ambavyo Mahita amekazania kuvionyesha, na hata kama ingekuwa ni visu tanataka wahusika wafikishwe mahakamani na siyo kuishia kuonyesha visu katika televisheni mbona watuhumiwa hawakuonyeshwa!

Si nia ya makala hii kukitetea chama cha CUF la hasha bali nasisitiza umuhimu wa mkuu wa jeshi la polisi kufuata sheria na taratibu za nchi hii, hivyo ndiyo utawala bora unavyotaka mambo yaendeshwe , Bila kuingia ndani, vitendo vya ujambazi mitaani,katika mabenki,kwenye magari, na mahali popote havichagui chama Fulani, mfano wizi wa NBC LTD huko Moshi,CRD LTD Tawi la Azikiwe Dar es salaam,NBC LTD Ubungo,Uporaji katika duka la vito Kariakoo,Wizi katika duka la kuuza fedha za kigeni nk Pia majambazi yamekuwa yakifanya uhalifu sehemu mbali mbali za nchi kama vile huko katika msitu wa Bihalamulo,Ngara,Karagwe, Kigoma, Mwanza, Arusha, Mbeya ,n.k huko kote majambazi yaliua na kupora mali za wananchi mbali mbali pasipo kuuliza uanachama wa chama chochote, majambazi wanaweza kutoka katika chama chochote kiwe cuf,ccm,chadema tlp n.k na wanapoamua kuua au kupora hawangalii uanachama wa ntu yeyote wao wanachotaka na fedha na mali tu.

Inaonekena Afande Mahita kaishiwa mbinu za kukabiliana na changamoto zinazolikabili jeshi la polisi kwa hivi sasa na anatafuta mbinu rahisi na hatari ya kuhusisha ujambazi na siasa za vyama na kwa njia hiyo anafikiri ataweza kuungwa mkono na wabunge,madiwani na serikali iliyoko madarakani!

Kama Mahita anafikiri hivyo atakuwa amapotea na amekosea sana, hakuna anayeweza kukubaliana na hoja dhaifu kama zake, wananchi kwa ujumla hawako tayari kukubaliana na sentesi za kiujulma kama zake,Pole sana Mahita hakuna aliye tayari kuingia katika mtego wako,dunia ya sasa watu hawaburuzwi na kauri za viongozi,dunia ya sasa inawapa nafasi wananchi kufikri na kutafakari kwa kina kabla ya kumuunga mkono mtu.

Kauri ya Afande Mahita imelihabisha na kuridhalilisha jeshi la polisi mbele ya umma wa watanzania, jamii haikutarajia kiongozi wa chombo kikubwa kama jeshi la polisi kutoa kauri ya kiujumla jumla kama yake.

Afande Mahita aelewe kuwa inawezekana kuwa sauti,muonekano, makeke n.k ya kupambana na uhalifu bado anavyo na vinazidi kuongezeka kila kukicha lakini ni ukweli ulio wazi kuwa akiri,mikakati, mbinu za kupambana na ujambazi vinaonekana kupungua kadri siku zinavyokwenda, jamii haina uwezo wala nguvu za kisheria za kumwambia ajiuzuru lakini ukweli unabaki pale pale kuwa sifa za kuendelea kuitwa mkuu wa jeshi la polisi Tanzania zinaonekana kupungua kwa kasi ya ajabu sana.


Huu ni mchango wa mawazo kwa kauri ya mahita.Makala hii ilitoka katika gazeti la Tanzania daima
innokahwa@yahoo.com

KWA MWENENDO HUU TTCL ISINGEWEZA KUIMILI VISHINDO VYA SIMU ZA MKONONI

Simu ni chombo cha mawasiliano, kwa muda mrefu kabla ya mageuzi ya sera za biashara na uchumi hususan sera ya mawasiliano hapa nchini Tanzania, mawasiliano yalitegemea sana simu za mezani(land line/fixed line) ambazo zilikuwa zinatolewa na kampuni pekee ya simu Tanzania(TTCL), baada ya mageuzi ya sera ya mawasilino tumeweza kushuhudia makampuni ya simu za mkononi yakiruhusiwa kuingia nchini na kuleta ushindani wa kibiashara.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za miaka kumi zilizopatikana kuanzia mwaka 1994 mpaka 2004 zinaonyesha idadi ya wateja wa simu za mezani walikuwa kama ifuatvyo:
88,325 (1994),90,270(1995),92,760(1996),105,095(1997), 121769(1998),149934(1999),171,617(2000),105,095(2001),161,797(2002),
146, 999(2003),146,414)2004).

Kwa kuangalia idadi hiyo hapo juu inaonyesha kuwa kampuni ya TTCL wateja wake wamekuwa wakiongezeka na kushuka, hakuna mabadiliko makubwa ya wateja hususan kuongezeka kama ambavyo ingetarajiwa, mfano mwaka 2004 TTCL inaonekana kuwa na wateja wa simu za mezani wapatao146,414 ukilinganisha na idadi ya wateja wa simu za mikononi kwa mwaka huo ilikuwa kama ifuatavyo Mobitel wateja 300,000,Celtel 700,000,Voda Com 1,200,000,hii ni katika kipindi kipindi kisichozidi miaka kumi tangu makampuni hayo yaingie sokoni.

Katika biashara yoyote mteja ni chazo kikuu cha mapato, hivyo ni jukumu la kampuni kuhakikisha kuwa inakuwa na wateja wengi kadri inavyowezekana,kwa kuhakikisha kwanza inabaki na wateja wake wa zamani,na pia kuvutia weteja wengine wapya.

Biashara ya simu hivi sasa ina ushindani mkubwa sana ulimwenguni kote hasa kutokana na ugunduzi wa teknolojia ya kisasa na rahisi ya mawasilino, hii ni changamoto kwa menejimenti na wafanyakazi wote kwa ujumla wa kampuni kuhakikisha kuwa ni kwa jinsi gani inaweza kupunguza ushindani na hivyo kubaki katika soko, katika soko la sasa la ushindani ni kampuni yenye kuweza kumrizisha mteja ndiyo itabaki.

TTCL inaweza kufanya mambo yafuatayo ili kuweza kubaki katika soko, kwanza ni kuimarisha huduma zinazotolewa na kampuni kwa mfano katika kipindi cha miaka mitano uwezo wa kampuni umekuwa kama ifuatavyo (capacity/line) mwaka 2001 njia 378,561, 2002 njia 234,419, 2003 njia 234,269, na mwaka 2004 njia 285,439 huu ni uwezo tu maana njia nyingi kati ya hizi zimekuwa hazifanyi kazi kwa sababu mbali mbali ndio maana katika mwaka 2004 imeonyesha kuwa kampuni ilikuwa na wateja 146,414 kama nilivyo eleza hapo mwanzo, hivyo basi ili kampuni iweze kuhimili vishindo vya simu za mkononi inabidi iwe na njia nyingi kwa kadri inavyowezekana maana njia ndio biashara yenyewe.

Pili, kampuni iweke mkakati wa kuongeza njia za wateja kwani kutokana na kutokuwepo kwa njia za kutosha imesababisha kuwepo mlundikano wa maombi mengi ya wateja wanaohitaji njia, mfano katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2001 mpaka 2004 mlundikano ulikuwa kama ifuatavyo mwaka 2000 wateja 14,375, mwaka 2001 wateja 5,518 mwaka 2002 wateja 7,183 mwaka 2003 wateja 7,183 na mwisho mwaka 2004 wateja 7,183 haya ni maombi ya wateja waliokuwa wanasubiri kupewa njia na hali ilikuwa mbaya sana kabla simu za mkononi kuingia katika soko kwa mfano mwaka 1995 wateja waliokuwa wanasubiri kupewa njia walikuwa wapatao 117,980 idadi inaonekana kupungua baada ya simu za mikononi kuingia katika soko na hivyo kuwafanya baadhi ya wateja kukosa mvuto wa kutumia simu za mezani ni vyema kampuni ikahakikisha kuwa kunakuwa na njia za kutosha na wateja hao wanahudumiwa vizuri, na inaweza kufanyikiwa kwa kuliangalia soko na kuligawa katika makundi( market segmentation) na hivyo kuweza kulihudumia kundi kutokana na mahitaji yake,pamoja na kuwa jitihada zimefanyika hasa baada ya kuanzishwa simu za malipo kabla(prepaid) ambapo muda wakusubiri hivi sasa umepungua inachukua siyo zaidi ya siku saba kupata njia ni maoni yangu kuwa huduma hii ya malipo kabla isambazwe Tanzania nzima kulikoni ilivyo hivi sasa ambavyo ni mikoa michache sana yenye huduma hii.

Tatu ni kusambaza vituo vya kupigia simu(callbox) hii ni moja wapo ya njia ambayo kampuni inaweza kutumia kwa kutoa huduma kwa wananchi wengi wasiyo kuwa na uwezo au wasiyo taka kuwa na simu za mezani kwani vituo hivyo vitakuwa vinatumika na wateja kupiga simu sehemu mabali mbali na kuingizia kampuni mapato ya kutosha, vituo hivyo inabidi visambazwe sehemu nyigi na kuhakikisha kuwa kadi za kupigia simu zinapatikana wakati wote na pia viwe vinafanyakazi muda wote.

Nne katika biashara ya ushindani bei ni kitu muhimu sana, bei ndio msingi mkuu wa uzarishaji wa faida ya kampuni ,kuna njia tatu ambazo kampuni inaweza kutumia kwamza ni kuangalia gharama ya uzarishaji wa huduma husika na kuweka faida(profit margin),pili ni kaangalia bei za washindani katika soko(competition oriented pricing) na mwisho ni kupanga bei kutokana na soko(market oriented pricing) hivyo ni vyema TTCL ikaangalia bei zake na hatimaye kuzifanya kuwa kivutio kwa walaji wake.

Watanzania walio wengi ni watu wenye kipato cha chini hivyo kwao bei ni kitu cha msingi sana kabla hawajafanya uamuzi wa manunuzi yoyote, ni bei gani itakuwa kivutio kwa mtumiaji wa simu za mezani hiyo ni jukumu la kampuni husika kufanya utafiti.

Tano ni upatikanaji wa huduma husika kwa muda husika ,katika huduma kinacho uzwa ni huduma ambayo ina sifa zifuatazo kwanza haigusiki,haiifadhiki,haidumu kwa muda mrefu,haijaribiwi,inapozarishwa papo hapo inatumika, n.k kutokana na sifa kama hizo ambazo ni kinyume na bidhaa zisizo za huduma hukuna budi kuhakikisha huduma ya simu inapatikana muda wote na kwa kiwango kinachoridhisha mteja ,matatizo ya kukatikakatika kwa mawasiliano kutokana na sababu mbali mbali ni sababu tosha ya kukosesha mteja, hivyo basi ni vyema kampuni ikaanza kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasilino kwa mfano sehemu nyingine kukosekana kwa mawasiliano imetokana na eidha kuanguka kwa nguzo au kuibiwa kwa waya, tatizo kama hilo linaweza kuondolewa kwa kutumia teknolojia isiyo tumia waya(wireless).

Sita ni matangazo na promosheni kuna msemo unaosema kuwa biashara ni matangazo, ni kweli matangazo ni njia ya kampuni kuwasiliana na mteja juu ya upatikanaji wa bidhaa fulani, ukiangalia jinsi kampuni za simu za mkononi zinavyojitangaza basi ni matarajio kuwa kampuni ya simu ya TTCL itajifunza kwa hilo njia kama radio,magazeti,televisheni,mabango,udhamini wa hafula mbali mbali,kusaidia jamii n,k matangazo ni uwekezaji(investment) inayolipa kwa muda mfupi na mrefu pia.

Mwisho ni kuwa biashara ya ushindani inamuweka mlaji katika nafasi nzuri kwaza anakuwa na taarifa nyingi juu ya bidhaa mabali mbali zilizoko katika soko,pia anakuwa na wigo mpana wa kuchagua ni bidhaa gani anunue ndio maana katika hali kama hiyo mteja anakuwa mfalme hivyo kampuni iliyojiweka sawa na kuwa tayari kumuhudumia mfalme ndio pekee atabaki katika soko.
Makala hii ilitoka katika gazeti la Tanzania daima mwaka jana

MNYONGE MYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI,UCHUMI WA TANZANIA UNAONEKANA KUKUA CHINI YA AWAMU YA TATU

Kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake juu ya utawala wa rais Mkapa 1995-2005 hususan juu ya uchumi wa Tanzania, lakini itakuwa siyo kumtendea haki na ni kupotosha umma kudai kuwa maendeleo ya Tanzania yanarudi nyuma.

Tunaweza kutofautiana ni kwa kiasa gani uchumi wa Tanzania umekua au ni kwa kasi gani ulitakiwa kukua lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa rais Mkapa anastahili pongezi kwa kuupa mwelekeo uchumi wa Tanzania.

Makala nyingi zimeandikwa zikichambua uchumi wa Tanzania chini ya awamu ya tatu ni maoni yangu kuwa tujenge tabia ya kuheshimu na kukubaliana ya vitu vyenye hoja za kitalaamu,kila taaluma ina umuhimu wake katika jamii,mwanatheolojia anapotoa hoja za kitaalamu ni vyema kama huna hoja yenye msingi wa kitalaamu ukaa kimya vivyo hivyo mwanahistoria akitoa uchambuzi kwa msingi wa kitaaluma ni vyeme ukatoa hoja za kitaaluma iedha kumuunga mkono au kumpinga vivyo hivyo kwa mwanauchumi, haipendezi na haikubaliki kukataa au kubeza kitu eti kwa kuwa akili au uhelewa wako haukubaliani nacho bila kuwa na msingi wa kitaaluma.

Katika uchumi kuna aina mbili kuu za kuanaglia uchumi wa nchi, kwanza ni uchumi mpana (macro economy) na pili ni uchumi mdogo (micro economy) si sahii kukataa kuwa uchumi haujakuwa eti kwa kuwa uchumi mpana haujaendana kwa kiwango sawa na uchumi mdogo.

Kwanini uchumi wa Tanzania umekuwa?ni kwa sababu nyingi kwa ajili ya makala hii zitatajwa chache tu zifuatazo:

Kwanza kushuka kwa mfumuko wa bei(inflation) kutoka asimia therathin na sita(36%) mwaka 1992 mpaka asilimia 4.8 mwaka 2005,tunaweza kutofautiana kuwa kiwango hicho hakitoshi au si kweli kuwa mfumuko wa bei umeshuka kiasi hicho au bidhaa na huduma zinazotumika kupima mfumuko wa bei si sahii n.k hayo ni maswala ya mjadala ukweli unabaki pale pale kuwa kushusha mfumoko wa bei kutoka katika tarakimu mbili(two digit) mwaka 1995 mpaka tarakimu moja (single digit) 2005 ni jambo zuri kiuchumi kwa mwananchi wa kawaida na kwa mwekezaji wa ndani na nje ya nchi, kwa kuwa mfumuko ukiwa juu maana yake ni kuwa pesa nyingi zinanunua vitu vichache sokoni, hakuna kigezo chochote kinachoweza kubeza ushushaji wa mfummuko wa bei kiasi hiki cha asilimia 5,hongera rais Mkapa kwa hili uongozi wako 1995-2005 unaiacha nchi ikiwa na kiwango kizuri sana cha mfumoko wa bei.

Pili ni kukua kwa uchumi kwa asimia6.8 mwaka 2005 ikilinganishwa na ukuaji wa uchumi wa asilimia3.6 mwaka 1995, kiwango hiki ni kizuri na kinaridhisha na kutia moyo ikilinganishwa na ilivyo kuwa miaka 1990s japo kuwa inatakiwa kazi kubwa ifanyike ili uchumi ukuwe kwa asilimia 8 mpaka kumi kwa muda wa miaka kumi ili matunda hayo yaweze kuonekana moja kwa moja kwa mwanachi wa kawaida,pamoja na hayo hiyo haiondio ukweli kuwa ni mafanikio ya utawala wa rais Mkapa kuuwezesha uchumi kukua kwa asilimia 6.8 ikizingatia kuwa mmoja wapo wa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani ni China ambayo kiwango chake ni asilimia 8.2.

Tatu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani kutoka pesa za kitanzania 25 bilioni mwaka 1995 mpaka wastani wa bilioni 150 kwa mwaka 2005, nini maana yake kwa mwananchi wa kawaida? Kwanza ni kuiwezesha serikali kuwa na uhakika wa kulipia gharama zake pasipo kukopa kwenye vyombo vya fedha vya ndani na kuwezesha vyombo hivyo badala ya kuikopesha serikali pesa hizo zinaweza kukopwa na wananchi na makampuni ya ndani ya nchi na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi wa nchi,pili kuiwezesha serikali kuwa na uwezo wa kulipia gharama za mishahara ya watumishi wake kwa wakati husika, nini maana yake kwa mwananchi wa kawaida? Ni kuwa watumishi kama vile walimu,jeshi,polisi, mahakimu,mabwana na mabibi shamba,madakitari n.k wana uhakika wa kupata malipo yao kwa muda na kuwawezesha kutoa huduma zao kwa mwananchi,tatu serikali imeweza kupunguza deni lake la ndani ambapo makampuni mbali mbali ya ndani yaliyokuwa yanaidai kwa muda mrefu yamelipwa na ivyo kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya nchi kwani makampuni hayo uzitumia fedha kulipia huduma zilizopatika hapa nchini kama vile mishahara, malighafi n.k si hivyo tu hivi makampuni yanayotoa huduma kwa serikali yana uhakika wa kulipwa pesa zao ambapo ulipwaji huo unasambaa(multiplier effect).

Nne serikali imeweza kutenga shilingi za kitanzania kwa mwezi bilioni1.8 kwa ujenzi wa barabara kutoka makusanyo ya ndani, haitaji kuwa mchumi wa kiwango cha juu ili kutambua umuhimu wa barabara katika maendeleo ya nchi ,inashangaza sana mtu anapobeza ujenzi wa barabara kwa madai kuwa zinanufaisha wenye mitaji na magari! Umuhimu wa miundo mbinu kama hiyo ipo wazi kwani uwawezesha wananchi kusafirisha budhaa na wao wenyewe kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa urahisi na gharama ndogo, mfano kutokana na kukamilika kwa barabara ya Kyaka mpaka Mtukula(japokuwa najua haikujengwa kwa pesa za ndani) kwanza kumefanya nauri kutoka Kyaka mpaka Bukoba mjini ishuke kutoka shilingi 2000 mwaka 1997 mpaka shilingi1500 mwaka 2005, pili muda unaotumika kwa mwananchi kutoka Kyaka mpaka Bukoba mjini kwa hivi sasa mwananchi anatumia saa moja tu kwenda na kurudi na usafiri wa mabasi na gari ndogo upo wakati wote ikilinganisha na adha na shida ya mwaka 1985 ambapo ilimurazimu mwananchi wa Kyaka kuamuka alfajiri saa kumi au tisa ili kuwahi basi lililojulikana kama’’komputa’’ na ukilikosa kwa kukuta limejaa hakuna basi tena labda udandie malori ya mizigo hivyo ilimchukua mwananchi siyo chini ya masaa 16 kwanda na kurudi tena kwa kubahatisha sana , pia barabara za kawaida za vijijini(feeder road)zimejengwa kutoka Kyaka mpaka Kilimilile hii ni mpya haikuwepo kabisa hivi sasa kuna usafiri wa Bukoba mjini mpaka Kilimilile pia barabara ya Mwisa mpaka Mabale hizi zote zimejengwa katika awamu ya Mkapa kwa mpango wa wa TASAF kwa ujumula barabara za rami zenye urefu wa kilometa 4700 na za kawaida kilomita 80,000 zimeshajengwa nchi nzima mpaka hivi sasa, sasa hii si faida kwa mwananchi wa kawaida nenda Kyaka umuulize mwananchi umuhimu wa barabara hiyo kama atakwambia kuwa haoni faida yake, kwa kukaa Dar es salaam na kuandika kuwa barabara zinamnufahisha mwekezaji na wenye mitaji ni uandishi wa ajabu sana nchi hii unaojitokeza wa kutokuona jambo lolote zuri eti kwa sababu wewe binafsi haunufaiki au kwa kuwa limefanywa na serikali ambayo hauiungi mkono!

Nne bajeti ya huduma za jamii kutoka asilimia4.6 mwaka1999/2000 mpaka asilimia 8.3 mwaka2004/5,bajeti ya maendeleo(development budget) kutoka 0.5mwaka 1999/2000 mpaka 3.5 asilimia mwaka 2004/5 hayo yote yamefanyika katika utawala wa rais Mkapa na yanaoneka kwa mwananchi wa kawaida,

Inaposemwa maendeleo ya Tanzania yanarudi nyuma nashindwa kuelewa ni vigezo gani vinatumika? Mfano vvyuo vikuu na vile vinavyotoa elimu ya juu vimeongezeka kutoka 23 mwaka 1995 na kufikia 43 mwaka 2005 sambamba na uongezekaji wa wanavyuo kutoka wanavyuo 14,076 mwaka 1995 mpaka mwanavyuo 48,236 mwaka 2005 likiwa ni ongezeko la asilimia 250,

Tano ongezeko la vitega uchumi kutoka nje (FDI) vyenye thamani ya dola za kimarekani 50.2 milioni mwaka1995 mpaka milioni 250 dola za kimarekani mwaka 2004,pia vitega uchumi vya ndani ukujumulisha na vya nje vilivyoandikishwa ‘’Tanzania Investment Center’’(TIC) kwa miaka kumi yaani 1995 mpaka 2005 ni miradi ipatayo 2527 iliyozarisha nafasi za kazi zipatazo 500,000.pia ubinafishaji ambao baadhi ya wachambuzi wamekuwa wanaulalamikia umeweza kuokoa kiasi cha pesa za kitanzania bilioni 100 kwa mwaka zilizokuwa zinatolewa kama rudhuku kwa mashirika ya umma,ukiachilia mbali ya faida ya kodi,nafasi za ajira,teknolojia mpya ,mitaji n,k iliyoambatana na ubinafishaji,mfano halisi kutoka huko Kyaka kiwanda cha sukari cha Kagera ambacho kilishafungwa lakini kutokana na ubinafishaji kimeweza kuanza uzarishaji upya na kulete ajira kwa mkoa wa Kagera na mikoa jirani na kwa hivi sasa kina mpango wa kujitanua na kujenga kiwanda kipya baada ya kupata eneo jingine la Kitengule.

Sita ongezeko la akiba ya fedha za kigeni za kuweza kuagiza bidhaa nje kwa kipindi cha miezi tisa mwaka 2005 ukilinganisha na mwaka 1995 ambapo akiba ilikuwa ya kuweza kuagiza miezi miwili,fedha hizo utumika kuagiza mahitaji mbalimbali kutoka nje kwani hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kujitosheleza kwa mahitaji yake yote ya ndani.

Saba kiwango cha umasikini kimeanza kushuka kutoka asilimia 38.6 mwaka 1991/92 mpaka asilimia 35.7 mwaka 2000/1 na wale wanaoishi katika umaskini uliokithiri kutoka asilimia 21.6 mwaka 1991/2 mpaka asilimia 18.7,hayo ni baadhi ya mafanikio ya rais B.W.Mkapa kwa uongozi wake wa miaka 10 ,kuondoa umasikini ni mchakato edelevu ambao hautamalizwa na kizazi kimoja bali ni juu yetu sisi wananchi na viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa tarehe 14 Disemba kuongeza kasi ya maendeleo hatimaye umaskini uwe ni historia Myonge mnongeni lakini haki yake mpeni ‘’Bravo’’ rais Benjamin William Mkapa
Makala hii ilitoka katika gazeti la Tanzania daima mwaka jana,imeandaliwa na Innocent M.Kahwa

WAPIGA DEBE SERIKALI ILICHELEWA SANA KUWACHUKULIA HATUA

Kumekuwepo mjadala juu ya wapiga debe katika vituo vya daladala hususan jiji la Dar es salaam,kuna maoni tofauti wengine wakiunga mkono kuondolewa kwao na baadhi wakipinga, ,kwa wale wanaopinga kwa kuwa wanatumia uhuru wao wa kikatiba sawa, lakini hakuna mtumiaji wa usafiri wa daladala atakaye pinga kuondolewa kwao, inawezekana wale wanaoipinga serikali hususani jiji kuwaondoa si watumiaji wa usafiri wa umma.

Ni kweli kuwa hivi sasa Tanzania inatekeleza sera ya soko huria lakini ikumbukwe kuwa biashara huria siyo leseni ya kuwafanya watu waishi bila kufuata sheria na taratibu za nchi au miji na majiji, pia ni kweli kuwa nchi inakabiliwa na janga la ukosefu wa ajira miongoni mwa wananchi wake hususan vijana lakini hiyo siyo sababu ya kuhalalisha wapiga debe vituoni, kwani wapiga debe ni wahalifu kama wahalifu wengine na hawawezi kuhalalishwa kwa kisingizio kuwa wanatafuta pesa za kujikimu.

Duniani wakati wa kampeni vyama ujinadi kwa kuahidi kutatua matatizo kadha yanayoikabili nchi husika kama vile ,tatizo la ajira,rushwa,uchumi, mazingira,uhalifu,n.k hakuna chama chochote makini kitakacho jinadi bila kueleza kuwa iwapo kitachaguliwa na kuingia madarakani kitatatua matatizo kama hayo, tumeshuhudia hata kwetu vyama vyote vilieleza matatizo kam hayo na hususan ajira kikiwemo chama cha mapinduzi.

Pia ni vyema jamii ikaelewa kuwa tatizo la ajira ni tatizo lililopo dunia nzima ,tofauti iliyopo ni aina ya ukosefu wa ajira baina ya nchi na nchi,na hakuna serikali duniani iliyomaliza kabisa tatizo la ajira la hasha bali kinachofanyika ni kulipunguza, si nia ya makala hii kukubaliana na hali iliyopo hivi sasa bali nia yangu ni kulieleza tatizo na kulijua na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kukabiliana nalo.

Ni kweli chama cha mapinduzi kiliahidi kuwa kitaongeza nafasi za ajira zipatazo milioni moja,kuna wanao beza kuwa haiwezekani ni uhuru wao kufanya hivyo lakini ni vigezo gani wanavitumia kubeza sijui,tunahitaji vigezo vya kitaalamu na wala siyo, hisia, kwa kuangalia Tanzania,maliasili,jiogorafia yake inapakana na nchi nane, bahari,idadi ya watu,utulivu wa kisiasa,utengemavu wa uchumi mkuu nk naona kuna uwezekano wa kuwa na nafasi zaidi ya hizo zilizotajwa na ccm.

Kwa watu makini ineeleweka kabisa kuwa kupatikana kwa nafasi za kazi ni mchakato na siyo swala la siku moja tu na wala haitarajiwi nafasi kama hizo ziwe zile za kuajiriwa serikalini,serikali inachotakiwa ni kujenga mazingira na fursa hivyo ni jukumu la mtu binafsi kutumia fursa hizo na hapa izingatiwe kinachotakiwa ni fursa halali.

Ni jambo la kusikitisha kuwa baadhi yetu tuna amini kuwa ni jukumu la serikali kukufanyia kila kitu kana kwamba serikali ina uwezo wa kimiujiza,

Ukiangalia wapiga debe wa mjini Dar es salaam hususan hawa wa vituo vya daladala, hakuna mtu makini anayeweza kuwaunga mkono wawepo kwa hali kama ilivyo hivi sasa, kwanza hawatakiwi na hawakubaliki na makondakta na madereva wa daladala na hvyo malipo yao ni ya kulazimisha yakiambatana na vitisho,ubabe na vurugu za kila aina, muulize dereva au kondakta yeyote juu ya watu hawa utapata jibu, kesi kadha zimeripotiwa katika vyombo vya habari juu ya kuchomana visu na wakati mwingine kuuana wakati wa kudaina malipo, kaulize kwa chama cha wenye daladala juu ya watu hawa,pia ni kero na wasumbufu kwa wasafiri na mwisho hakuna chombo chochote kinachowatambua bali wanalazimisha tu.

Kinachoitwa ajira ya wapiga debe mjini hakikubaliki hii siyo ajira ,ajira lazima iwe halali na lazima pawepo na makubaliono ya hiyari kwa pande zote, kwanza ni kuongeza gharama za uendeshaji bila sababu za msingi hebu angalia mfano ufuatao, abiria anaamuka asubuhi anaenda katika kituo cha daladala cha Rozana kilichopo Buguruni ili akapande daladala la kwenda Posta au Kariakoo pale kituoni anakuta msululu wa abiria wakisubiri basi na linapofika wanasukumana na kugombea ili kuweza kuingia ndani na kupata nafasi na siyo kukaa maana kukaa wakati wa asubuhi ni anasa sasa katika mazingira kama hayo mpiga debe wa nini na analipwa kwa kazi gani, maana kwa wakati huo magari ni machache kuliko abiria lakini utaona kundi la wapiga debe kibao! hii ndiyo tunaita ajira?

Si hivyo tu bali hata wakati wa mchana ambapo abiria wanakuwa wachache na magari kuwa mengi bado wapiga debe hawahitajiki maana kazi ya kuvutia abiria inaweza kufanywa na deriva pamoja na kondokta wake, kinachohitajika ni hawa makondakta na madereva kupewa semina ili kujua abc za uendesahji wa daladala ,napendekeza chama cha wanye dala dala waendeshe semina za kuwaelimisha madereva na makondakta na hivyo kuwafanya waweze kuendesha kistarabu zaidi na kwa gharama nafuu, maana wakati mwingine gharama za uendeshaji zinaongezwa na ukosefu wa elimu ya msingi ya biashara ya daladala, gharama zinazotokana na faini,rushwa,ajali,uharibifu wa gari na kuchakaa mapema,gharama ya wapiga debe n,k vyote hivyo vinaweza kuepukwa na hatimaye kumpunguzia abiria gharama za usafiri.

Kwa kuwa na waedeshaji wenye elimu ya biashara ya daladala hakuna haja ya kuwa na wapiga debe kwani kazi hiyo itafanywa na kondakta na dereva, mfano wakati wa asubuhi kondakta anaweza kutumika kuwapanga abiria ili wapande gari kwa kufuata utaratibu maalumu wakati huo kukaanzishwa utaratibu maalumu wa mabasi kuegesha vituoni na kutakiwa gari la kwanza ndilo linaanza kupakia(first in first out) na vitu kama hivyo.

Nchi zote ulimwenguni zina matatizo yanayotofautiana kutokana na tofauti ya maendeleo,mazingira,tamaduni,historia n,k na ni kweli kuwa matatizo ni zao la jamii husika,lakini pia kuishi ni mchakato ambao uzaa na kuibua matatizo kulingana na wakati, hivyo ni jukumu la jamii kushughulikia tatizo kadri linavyojitokeza.

Tatizo nilionalo na ambalo rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin W.Mkapa aliwahi kuligusia ni kuwa kuna hatari ya kujenga taifa la walalamishi tu,wachambuzi wengi wamekuwa wepesi wa kulaamu tu tena ni hodari sana lakini kulaumu siyo sululisho ni vyema tukawa tunalaumu na kutoa sululisho.

Katika kutatua tatizo kuna hatua kuu zifuatazo kwanza ni kuhainisha tatizo(problem identification) hapa tuna tatizo la ajira mjini na vijijini,wapiga debe ni matokeo ya tatizo la ajira kwa upana wake, hivi sasa mijini kuna vijana ambao hawana ajira na matokeo yake wanatafuta njia rahisi ambazo wanafikiri kuwa ni ajira mfano,wapiga debe,machangu doa,majambazi,n,k kumbe hizo siyo ajira bali ni uhalifu kama uhalifu mwingine ambao unaadhibiwa mbele ya sheria,jambazi hawezi kuhalalisha ujambazi wake kwa kisingizio kuwa serikali haijampatia ajira na hana njia nyingine ya kuweza kumfanya aweze kujikimu kimaisha,vivyo hivyo kwa wapiga debe hawatikiwi na wenye magari,hawatikiwi na abiria na mwisho jiji haliwatambui kwahiyo ni vyema wapiga debe tuwaangalie kwa mtazamo huo.

Hatua ya pili ni kuangalia njia mbadala(alternatives solutions) za kuweza kuondoa tatizo husika,hapa kuna njia kuu mbili kuna zile za muda mrefu kama vile MKUKUTA,MKURABITA,MMEM,MMES,urekebishaji wa uchumi,ujenzi wa vyuo vikuu na vya ufundi ,ukaribishaji wa vitega uchumi,uhanzishaji wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa,ujenzi wa miundo mbinu n,k, pia kuna njia za muda mfupi kama vile kuwaelimisha wapiga debe ili wajue kuwa vitendo vyao siyo ajira bali ni uhalifu,kuwaondoa,kuwapatia mashamba, kuwahimiza wajiunge katika vikundi vya uzarishaji mali, kuwapeleka katika mafuzo mbali mbali ,kuwaingiza katika mfumo rasmi na hivyo kutambuliwa kwa kazi yao kama ajira na washika dau wa usafiri mijini na hvyo kazi hiyo kuendeshwa kwa utaratibu maalumu wenye kuelewaka na usiyo na kero kwa pande zote n.k

Hatua ya tatu ni kuchagua njia muafaka (selecting best alternatives) kati ya zilizo tajwa katika hatua ya pili, hii inategemeana na rasilimali zilizopo,ukubwa wa tatizo,muda , uharaka, mazingira n.k

Hatua ya nne ni utekelezaji(implementation), njia zilizoteuliwa kutatua tatizo utekelezwa, na hapa ndipo ujitokeza watu wengi wa kulaumu utekelezaji pasipo kutoa njia mbadala ambazo wanafikiria kuwa nzuri zaidi.

Hatua ya mwisho ni mshindo nyuma(feedback) baada ya utekelezaji ni vyema ikafanyika tathimini ili kujua kwa kiasi gani tatizo limeweza kutatuliwa na kama la kwa nini?.

Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa swala la wapiga debe kama matatizo mengine lililvyoachwa kwa muda mrefu bila kushugulikiwa na linaposhugulikiwa inakuwa siasa mno,inawezekana jamii ilishaaza kuliona kuwa ni jambo la kawaida ,mazoea yana taabu, Mfano kuna wizi wa vifaa vya magari kama vile tairi,vioo,radio,taa nk ambao ufanyika Dar es salaam na vifaa hivyo kupelekwa kidongo chekundu(gerezani) ambapo mwenye kifaa kilicho ibiwa utakiwa kukinunua tena kifaa chake kutoka kwa wezi au mawakala wa wezi hao na unapojaribu kutoa taarifa polisi kama ni kioo kinaweza kuvunjwa mbele ya macho yako na hakuna hatua zinazochukuliwa na imefikia hatua ya wenye magari kuona hilo ni jambo la haki na la kawaida na hivyo mtu kununua kifaa chake ni jambo la kawaida,sijui kwa siku za karibuni na hasa kasi mpya kama hali imebadilika lakini ninachotaka kueleza kuwa kuna hatari jamii ikikata tamaa na kuzoea uhalifu na kuona wa kawaida ,serikali ilichelewa kuchukua hatua dhidi ya wapiga debe na hatua zilizochukuliwa ni muafaka za kuwaondoa.

Makala hii iliwahi kutoka katika gazeti la Tanzania daima
innokahwa@yahoo.com
Tel +255744292718

TANZANIA TUNAWEZA KUJIFUNZA NINI KUTOKA KWA NCHI ZINAZOJULIKANA KAMA CHUI WA ASIA YA MASHARIKI(EAST ASIAN TIGERS)?

Tanzania ni chi maskini sana kwa mujibu wa vigezo vya Shirika la fedha ulimwenguni(IMF) na benki ya dunia, lakini umaskini wa nchi hii si wa ukosefu wa rasilimali bali kimsingi ni umaskini unaosababishwa na kutokuwa na viongozi wenye visheni na pia wananchi wenyewe kutokujua kuwa wanaweza kuufanya umaskini kuwa historia.

Ukiangalia baadhi ya nchi ambazo wakati Tanganyika inapata uhuru wake mwaka 1961,maendeleo ya nchi hizo yalikuwa kimsingi sawa na Tanganyika, nchi hizo kama vile Korea Kusini, Hong kong,Singapore na Taiwan, swali la msingi la kujiuliza ni kwa sababu gani nchi hizo zimeweza kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo? Je Tanzania tunaweza kujifunza nini?

Kwanza ni mkazo katika elimu,nchi hizi ziliweka sana mkazo mkubwa katika kuwekeza katika sekta ya elimu, kwa mfano mpaka mwaka 1980 kulikuwa na wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu katika fani ya uhandisi nchini Korea Kusini ambao idadi yao ni sawa ukijumlisha wahitimu wa nchi za Ujerumani,Sweden na Ufaransa kwa pamoja!

Pia nchi hizo hazikukazania wingi tu wa wahitimu bali ubora ulitiliwa sana mkazo kiasi kwamba wanafunzi wa Korea Kusini na wa kutoka nchi nyingine hizi kama Singapore, Hong kong,na Taiwan ni bora kuliko wanafunzi wa Marekani katika masomo ya hisabati(mathematics) na Sayansi, sasa sisi kama Taifa tuna mikakati gani ya kufanya ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wakati huo huo tukihakikisha ubora wa wahitimu wetu wanaohitimu katika vyuo vikuu na elimu ya juu pasipo kusahau elimu ya sekondari na msingi.

Kwa kufanya hivyo tunaweza kupiga hatua kubwa sana katika maendeleo,kama kweli tumeamua kuufanya umaskini kuwa historia hatuna budi kuwekeza katika elimu na hakuna njia ya mkato, dunia ya sasa iliyo jaa ushindani inahitaji watu walio elimika kwa kiwango cha kimataifa na ukizingatia dunia ya sasa ambayo haitambui mipaka ya nchi umuhimu wa ubora unakuwa na nguvu zaidi.

Ni jukumu la serikali iliyoko madarakani hivi sasa kuhakikisha kuwa vijana wengi kadri inavyowezekana wanapata nafasi za kusoma, hivyo hivyo mwananchi mmoja mmoja na katika makundi kuhakikisha kuwa elimu inakuwa ndiyo kipaumbele chetu, kama tunaweza kuchangia michango mikubwa katika harusi kwanini tusikinusuru kizazi na nchi yetu kwa kuchangia ujenzi wa shule na vyuo?

Inawezekana kabisa kupiga maendeleo makubwa iwapo wananchi watahamasishwa kufanya hivyo, kama wenzetu wameweza kwa nini sisi tushindwe? Wakati ni huu wa kuibadili Tanzania na kamwe tusitarajie miujiza.

Pili ni uwekaji wa hakiba(a high savings level) hususan katika miaka ya 1960s na 1970s serikali za nchi zilizotajwa hapo juu ziliweza na kufanyikiwa kuwahimiza sana wananchi wao kuweka hakiba ya fedha zao na kuwazuia kutowekeza nje ya nchi, pia nchi hizo zilipunguza uagizaji wa bidhaa toka nje ya nchi na kuweka kodi kubwa kwa bidhaa za kulika(consumers goods),wananchi waliweka pesa zao benki na benki zilitumia pesa hizo kukopesha kwa kutoza riba ndogo kwa ajili ya uwekezaji katika uzarishaji na biashara,

Kutokana na sababu hiyo inahitajika jitihada kubwa sana kuwawezesha watanzania kuwa na utamaduni wa kuweka pesa benki kwani ni watanzania wachache sana wenye desturi ya kutunza pesa zao benki, sababu inayotolewa ya kipato kidogo si sababu ya msingi kwani watu hao hao wanaodai kuwa vipato vyao ni vidogo utawakuta wanaendesha magari ya kifahari,kunywa pombe na starehe nyingine nyingi za kuonyeshana ufahari n.k. hizo zote ni dalili za ukosefu wa utamaduni wa kuweka akiba benki, watazania walio wengi wanapenda kuiga utamaduni wa kimareakni wa kutumia hata kama ni kuingia madeni!

Katika hali kama hii nchi haiwezi kupiga maendeleo makubwa, kinachotakiwa siyo lazima uweke pesa nyigi kwa mkupuo, kwani waenga walisema kuwa ndoo ndoo si chururu au haba na haba ujaza kibaba hizo ni methali zenye kuimiza utamaduni wa kuweka hakiba,

Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa hata wafanyabishara wetu hawana utamaduni mkubwa wa kuweka pesa benki matokeo yake ni kusikia majambazi yamevamia na kuiba mamilioni ya fedha majumbani

Si wafanyabiashara tu bali hata viongozi wetu hawana tabia ya kuweka pesa benki ndiyo maana wakati wagombea urais,ubunge hata udiwani walikuwa wanatumia pesa tasilimu wakati wakiwasilisha michango/ada ya kuchukua fomu, kwa mfano katika ccm wagombea urais walitakiwa kulipa milioni moja kama ada na zilitolewa pesa tasilimu hicho ni kielelezo cha kutokuwa na utamaduni wa kutumia benki na hii si kwa ccm tu bali vyama vyote havikuwa vinatumia benki kupokea michango au ada kama hizo, hii inaonyesha jinsi tatizo la kutotumia benki lilivyo kubwa .

Katika biashara ya benki pesa zinazotolewa kama mikopo uwa ni amana za wateja wengine, natambua kuwa kuna amana za makampuni lakini hiyo haiondoi umuhimu wa amana za watu binafsi,sasa unatarajia nini ikiwa watu watakuwa hawana utamaduni wa kuweka pesa benki? Matokeo yake ni kuwa na amana kidogo katika benki na kusababisha riba kuwa kubwa kwa kuwa wanaotaka kukopa ni wengi kuliko pesa zinazowekwa na wateja pamoja na kuwa kuna sababu nyingine zinazosababisha riba kuwa kubwa ikiwepo mfumuko wa bei na hatari inayoambatana na mkop(risk)

Kama kweli tunataka maendeleo ni vyema vikwazo vyote vinavyosababisha wananchi wasiweke pesa zao benki vipunguzwe kama siyo kuondolewa kabisa,

Tatu ukiangalia ulali wa biashara(balance of trade) ni hasi,tuna agiza bidhaa nyingi kuliko zinazopelekwa nje, matokeo yake ni kutumia fedha nyingi za kigeni, na wakati huo huo ni kuimarisha viwanda vya nchi nyingine na kuongeza ajira katika nchi za nje, kwahiyo jitihada kubwa inabidi zifanyike kubadili hali hiyo .

Pia ukiangalia bidhaa zinazoingizwa nchini ni bidhaa za ulaji na siyo za uzarishaji kama vile mashine na mitambo ya kuzarisha mali, kwahiyo ni vyema tukaimarisha viwanda vya ndani ambavyo vatazarisha mali zitakazoweza kutumika hapa nchini na ziada kupelekwa nje na kuingiza pesa za kigeni tunaweza kulinda viwanda vyetu kwa kuweka kodi kubwa na hii itasaida pia kulikinga taifa letu lisiwe dampo ya bidhaa toka nje


Nne ni kujikita katika uuzaji wa bdhaa nje ya nchi, nchi hizi zilifanyikiwa sana kuweka mikakati mahususi ya kuziwezesha kuuza bidhaa nje ya nchi(export- driven) serikali za nchi hizo zinafanya kila liwezakanalo kusaidia viwanda kuuza bidhaa nje ya nchi zinazozarishwa nchini mwao, kwa mfano mameneja na wafanyakazi wanafundishwa kuzarisha bidhaa zinahitajika katika soko la nje na thamani ya pesa ya nchi hizi inawekwa chini ili kuziwezesha bidhaa zao kuweza kuuzwa kwa bei ya chini nje na hivyo kupunguza au kuua ushindani katika soko la kimataifa, kwa muda mrefu pesa ya Tanzania yaani shilingi imekuwa ikishuka thamani lakini kwa bahati mbaya sana hatujaweza kunufaika na kushuka huko kwa kuwa nchi haina bidhaa nyingi za kuweza kuuza nje ya nchi.

Tanzania ina nafasi nzuri sana kuweza kufanya hivyo ,kwanza jiogorafia ya nchi inaiweka katika nafasi nzuri, nchi yetu imepakana na nchi zisizo pungua nane, pia tuna bahari na bandari ambayo ni kiungo kikubwa katika usafirishaji wa biashara za kimataifa.

Jitihada zinazoendelea za kuimarisha na kujenga maeneo mahususi kwa ajili ya uzarishaji(epz – economic processing zone na sez-special economic zone) inapidi zifanyike kwa nguvu na kasi kubwa kwani ndiyo ukombozi wa uchumi wetu kwa kufanya hivyo tunaweza kutumia nafasi yetu ya kujogorafia vizuri.

Masoko ya Umoja wa nchi za kusini mwa Afrika(SADC) na Afika mashariki(EAC), soko nafuu la Amerika(AGOA), soko nafuu la ulaya ambapo Tanzania inaruhusiwa kuuza ulaya bidhaa aina zote ukiacha silaha n.k

Hayo ni baadhi ya mambo ya msingi ambayo yanatakiwa kufanyika ili kweli kuwa na Tanzania ya neema,Makala hii iliwahi kutoka katika gazeti la Tanzania daima
imeandaliwa na innokahwa@yahoo.com
Tel 0744 292718

Saturday, April 15, 2006

KWA SABABU YOYOTE BADO BARAZA LA MAWAZIRI LA RAIS KIKWETE NI KUBWA MNO

Rais Kikwete ametangaza baraza lake la mawaziri na tayari limeapishwa na hivyo kuwawezesha mawaziri hao kuanza kazi kwa hari mpya,kasi mpya na nguvu mpya ili kujenga Tanzania yenye neema,baraza hilo lina jumla ya mawaziri 29, manaibu 31, ukijumulisha na waziri mkuu lina jumla ya mawaziri 61!.

Idadi hiyo kwa vyovyote vile ni kubwa mno si kwa kulinganisha na serikali za awamu zilizopita la hasha bali kwa kuchambua majukumu ya waziri na manaibu wao.

Swali la msingi ambalo tunapaswa kujiuliza ni je,kulikuwa na umuhimu wa kuwa na wizara na manaibu wengi kiasi hicho? Majibu ya swali hili yatapatikana kwa kusoma makala hii,

Kwanza kuna wizara hii mpya ya Ushirikiano wa Afrika mashariki,wizara hii ina waziri na naibu wake! Pamoja na umuhimu wa jumuiya hii bado hakukuwa na sababu za msingi za kuwa na wizara kamili na naibu wake hata kama Kenya na Uganda wanazo wizara kama hii bado si sababu za msingi za wizara hii kuwepo,

Ushirikiano wa jumuiya (EAC) ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu la Tanzania na ukizingatia swala la utandawazi ndipo umuhimu unavyozidi kwani jamuiya yenye nguvu kiuchumi ndio itakuwa na sauti ulimwenguni..

Katika jumuiya ya Afrika Mashariki kinachotengenezwa ni mazingira na fursa ambazo zina tarajiwa zitumiwe na nchi wanachama wake, pale haukuti ajira, soko,wala vitega uchumi bali inatengenezwa fursa ya kuweza kutumika kuzarisha ajira, soko n.k, kwa maana hiyo wajibu mkubwa upo ndani ya nchi husika, mfano katika jumuiya na hasa tutakapokuwa tumefikia katika umoja wa soko(common market) ambapo raia wa nchi moja ataruhusiwa kwenda kufanya kazi katika nchi nyingine pasipo kuwekewa vizingiti na masharti yoyote, hii ni fursa ya ajira lakini haitakuwa na maana yoyote kwa Tanzania kama wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na wizara ya elimu ya juu,sayansi na teknolojia zitakuwa hazikujiandaa vyema kwa kuzarisha watanzania wenye ujuzi,maarifa na elimu ambayo inawafanya kuwa washindani katika soko(competitive), vivyo hivyo jumuiya ni fursa ya soko lakini Tanzania tutanufaika kwa kutumia soko hilo kwa kuwa na bidhaa bora zinazoweza kuuzika katika soko hilo na hapo ndipo jukumu la wazara ya uchumi, mipango na uwezeshaji,fedha. Pia na viwanda na biashara n.k zinapokuwa na umuhimu katika mchakato wa kuwawezesha watanzania kunufaika na fursa zinazopatika katika jumuiya

Kwa kuangalia mambo kama hayo yaliyotajwa utaona kuwa mambo ya msingi yanayotakiwa kutunufaisha sisi watanzania yanatakiwa yafanyike ndani ya nchi yetu na hayo ni makumu ya wazara mbali mbali kwa umoja wao, kutokana na sabubu hizo bado hakukuwa na hoja ya msingi ya kuwa na waziri kamili na naibu wake,wa nini? Kwa nini jukumu hilo lisingefanywa na naibu waziri katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa?
Katika hali halisi hivi sasa, nini yatakuwa majukumu ya kila siku ya wizara? Matokeo yake tutakuwa na watu ambao hawana majukumu ya kila siku hivyo kupoteza pesa na rasilimali kadha ambazo zingeweza kutumika sehemu nyingine ambazo ni nyeti zaidi,mfano katika jumuiya hii iliundwa mahakama ya Afrika Mashariki(The East Africa Court of Justice) lakini kipindi chote hiki tangu iundwe haijawai kupokea hata shauri moja,

Pili hakukuwa na sababu za msingi za kuwa na manaibu waziri wawili katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Kimataifa, izingatiwe kuwa mawaziri si watendaji wakuu wa wizara bali ni wasimamizi tu, kazi zote za kitaalamu za kila siku zinafanywa na wataalamu waliopo wizarani,kinachoitajika kufanyika hapo wizarani ni kubadilisha akiri (mindset) za watumishi ili wajue majukumu mapya ya wazara ya mambo ya nje ni kuiletea nchi shibe kwa kuitangaza vizuri na kuimarisha ushiriano wa nchi na nchi pia na vyombo na taasisi za kimataifa ulimwenguni,siasa za longo longo hazitailetea nchi shibe.

Waziri na naibu wake mmoja tu anatosha kutekeleza majukumu ya wizara hiyo,baadhi ya kazi za msingi za wizara hii zinaweza kutekelezwa vizuri sana na barozi zetu zilizoko nje ikiwa zitapangwa vizuri.

Tatu wizara ya mambo ya ndani imetenganishwa na kuwa wizara mbili moja ikiwa wizara ya usalama wa raia na nyingine ikibaki kuwa wizara ya mambo ya ndani na zima moto, ni kweli serikali ya awamu ya nne haipaswi iwaache majambazi yatambe kwa kuiba mali za wananchi na kuwaua, lakini kama serikali inafikiri sululisho la tatizo hili ni kuundwa kwa wizara ya usalama wa raia itakuwa imekosea na imepotea sana.

Kuongezeka kwa matukio ya ujambazi nchini kuna sababu nyingi tu za msingi na hazina uhusiano wa moja kwa moja na muundo na ukubwa wa wizara, kama vile Ukosefu wa vitendea kazi ndani ya jeshi la polisi ,si hajabu kukuta walaya nzima ina gari moja la polisi au mawili tu,idadi ndogo ya watumishi(polisi),mishahara na marupu rupu madogo yasiyojenga na kuongeza tija(productivity),ukosefu wa vifaa na zana za kufanyia kazi,udhaifu katika mbinu za kisasa na mikakati(strategy) za kukabiliana na wahalifu n.k hayo yote hayataondoka kwa kuunda wizara tu, ni mambo yanayojulikana ndani ya jeshi la polisi na watendaji wote waliokuwa wizara ya mambo ya ndani bali hayakutafutiwa ufumbuzi kwa sababu ukosefu wa bajeti ya kutosha.

Pia uhalifu umeongezeka kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi,tamaa ya kuwa na mali pasipokufanya kazi,mmomonyoko wa maadili,muingiliano wa jamii mbali mbali,utandawazi n,k ni vyema swala hili likaangaliwa kwa mapana yake, hii inanikumbusha kisa kimoja kilicho simuliwa na Mhudhama Karidinari Pengo ambaye anasema kuwa katika pita pita yake mtaani Dar es salaam aliwakuta akina dada wanafanya biashara ya ngono(umalaya) alisimamisha gari na kuwauliza kuwa nyie hamuoni kuwa mnahatarisha maisha yenu kwa UKIMWI? Kina dada hao walimjibu kuwa ni heri kufa na UKIMWI kesho kuliko kufa na njaa leo, ninachotaka kueleza ni kuwa ni vyema tuka angalia sababu za msingi(root cause) za kuongezeka kwa uhalifu na tukapambana nazo badala ya kuangalia matokeo tu, sabubu hizo hizo ndizo zinapunguza ufanisi katika magereza,uhamiaji na zimamto n.k
Nne hakuna sabubu ya kuwa na waziri anaye shughulika na mazingira peke yake labda kama ni kuwafurahisha wafadhili na hivyo kuvutia misaada , kwa maoni yangu waziri mmoja tu angetosha kushughulikia, mazingira na mambo ya Muungano ,kwani ukiangalia kwa undani shughuli zote za uharibifu wa mazingira zinafanyika katika wizara mbali mbali, mfano kuna uharibifu mkubwa wa mazingira katika uchimbaji na usafishaji wa madini,Kilimo,Mifugo,Maji ,Mali ya asiri na Utalii,Makazi,Miundo mbinu n.k vivyo hivyo ni jukumu la wizara husika kuhakikisha kuwa shughuli zilizoko chini ya wizara husika zinalinda na kujenga mazingira kwa faida ya kizazi cha leo na kesho.

Pia Mambo ya Muungano yote yana wizara zinazowajibika kwa kila siku juu ya maswala ya muungano kama vile Wizara ya Fedha,Elimu ya juu,sayansi na teknolojia, Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa, Mambo ya nje na Ushirikano wa kimataifa, mambo ya ndani n.k ninachotaka kukieleza hapa ni kuwa shughuli zote zinazo husu muungano zina waziri muhusika anayewajibika nazo kila siku,

Kutokana na sababu hizo hakukuwa na haja ya kuwa na mawaziri wawili bali waziri mmoja tu angetosha kushughulikia mazingira kama mratibu tu na muunganishi wa wizra zote ili kuhaikikisha zinalinda mazingara pia vivyo hivyo angeweza kuratibu na kuwa kiunganishi ili kuhakikisha kuwa wizara husika zinatekeleza majukumu yao kulingana na mkataba wa muungano,Katiba na sheria za nchi zinazo husu muungano,kama nilivyoeleza hapu juu shughuli zote za kila siku zina mawaziri husika hivyo kumfanya waziri huyu kuwa na majukumu madogo ambayo anaweza kuyaghulikia yote mawili yaani mazingira na muungano.

Tano hakukuwa na sababu ya msingi kuwa na naibu waziri anayeshughulikia maafa na kampeni ya UKIMWI, shughuli za kampeni ya UKIMWI zinaweza kufanywa vizuri na wizara ya afya kama inavyofanya kwa magojwa mengine kama vile maralia,kipundu pindu,kisukari,Tb n.k,kweli ukimwi ni hatari, na maali pake ni wizara ya afya lakini pia ni ukweli ulio wazi kuwa maralia inaua watu wengi kuliko ukimwi inakadiriwa kuwa kila baada ya dakika Watanzania 5 wanakufa kwa maralia sasa kama ni kujali maisha ya watanzania basi maralia ndio ilipaswa kupewa naibu waziri. Naibu anayeshughukia bunge angeweza pia kushughulika maafa pasipo kuathiri ufanisi wa kazi.

Sita hakuna sababu ya kuwa na mawaziri wa nchi wawili mmoja akishughulikia Utawala bora na mwingine akishughulikia Siasa na uhusiano wa jimii,kimantiki yote hayo ndio utawala bora kwahiyo yange uganishwa na kuwa chini ya waziri mmoja,

Saba sioni sababu za msingi za kuwa na wizara ya kazi, ajira na maendeleo ya vijana na kuwa na manaibu wawili, kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa hapo mwanzo shughuli za wizara hii nyingi zinafanyika au kutekelezwa katika wizara nyingine , wizara hii imewekwa kisiasa mno, si jukumu na wala haitarajiwi wizara hii kuzarisha nafasi za kazi kwa watanzania, maana nafasi za ajira zitapatikana kwa uchumi kukua,viwanda kuazishwa,kilimo na mifugo kuboreshwa n.k hivyo shughuli haswa za kuzarisha ajira zipo katka wizara nyingine,pia vivyo hivyo maendeleo ya vijana kwa maana pana ,ni kupata elimu bora,ajira, afya safi na kwa ujumula maisha yenye neema na mambo yote hayo yanafanyika na kutekelezwa na wizara mbali mbali kwa ujumla wake,
Jukumu la kubuni sera,kutunga sheria na kusimimia sheria ya kazi yanaweza kutekelezwa kwa baadhi kuyahamishia wizara ya habari,utamaduni na michezo na mengine kuwa ni idara tu katika wizara nyingine.

Nchi hii ni yetu sote na tunalo jukumu la kutoa mawazo juu ya msakabali wa nchi yetu,ni mawazo dhaifu kusema kuwa tusubiri kwanza ili tuone utendaji wa baraza ndio tutoe maoni,hii ni falsafa mbaya ya kusubiri janga litokee ndiyo uanzae kulishughulikia ,waswahili usema heri nusu shari kuliko shari kamili,mimi kama mtanzania niliyebahatika kusomeshwa na nchi yangu ninao wajibu wa kuchangia mawazo juu ya ujenzi wa nchi yetu, mawazo haya siyo lazima yawe sahii kwa asilimia mia bali ni jukumu la kila mwananchi kuchangia mawazo juu ya maendeleo ya nchi yetu Tanzania, Nawatakia afya, fikra mpya za kuigeuza Tanzania kuwa yenye neema.

MKURABITA SIYO MUAROBAINI WA UMASKINI WA WANYONGE TANZANIA

Ili kuondoa au kupunguza umaskini uliokirithiri Tanzania ambapo wananchi wake wengi wanaishi katika umaskini uliotopea awamu ya tatu chini ya rais aliye ondoka madarakani B.J. Mkapa ilianzisha MKURABITA ambao ni Mpango wa Kurasmishisha Biashara ya Wanyonge wa Tanzania, mpango huu umeasisiwa na mtalaamu maharufu toka Peru anayejulikana kama Hernando de Sato ambaye ni rais wa “Institute for Liberty and Democracy’’, mtalaamu huyu anaamini kuwa mfumo wa ubepari umeweza kufanyikiwa na kufanya vizuri Amerika,Ulaya magharibi,Japan na katika nchi nne za Asia zinazojulikana kama ‘’four Asian tigers’ ambazo ni Hong kong,Korea kusini,Singapore na Tawain ni mfumo mzuri wa urasmishaji mali na sheria ambao uwezesha mali na biashara kutambulika kisheria na hivyo kuweza kuzitumia mali hizo kupata mikopo kutoka benki au taasisi za fedha, mtaalamu huyo anaamini katika thamani(value) iliyopo katika karatasi kwa maana ya hati kwani hati ndio itumikayo kama dhamana wakati wa kuomba mikopo.


Moja wapo ya lengo na madhumuni ya mpango wa kurasmisha mali na biashara ya wanyonge wa Tanzania ili hatimaye wanyonge hao waweze kuzitumia mali hizo kuweza kupata mikopo benki na katika taasisi za fedha(financial institution). Kutokana na tathimini iliyofanyika nchini inaonyesha kuwa asilimia 98 ya biashara zote zinzofanyika hapa nchini siyo rasmi na hivyo hazitambuliki kisheria, hivyo hivyo asilimia 89 ya mali zilizopo hapa nchini pia hazitambuliki kisheria,


Ukiangalia MKURABITA kwa makini utagundua mapungu yafuatayo ya msingi ambayo hakuna budi yafanyiwe marekebisho ili mpango huu uweze kuondoa na kupunguza umaskini nchini:

Kwanza mpango huu unaangalia tatizo la wanyonge kwa mtazamo hafifu au dhaifu kuwa ukosefu wa mitaji ndio msingi mkuu wa wanyonge wa Tanzania na tatizo hilo linaweza kuondoshwa kwa kurasmisha mali au biashara na kuwa na hati ambayo itatumika kama dhamana benki.

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwa mwanzilishi wa dhana hii De Sato ambaye anaamini kuwa mazingira na sababu zilizofanya ubepari ufanyikiwe katika nchi zilizotajwa hapo juu ndio hizo hizo zitafanya ufanyikiwe duniani kote na hususan Tanzania!

Ukiangalia mazingira ya katanzania ambapo asilimia 84 ya watanzania wenye uwezo wa kuzarisha mali wanajishughulisha na kilimo cha chakula na biashara ambao ni wakulima wadogo wanaotumia jembe la mkono na kutegemea majaliwa ya Mwenyezi Mungu kuleta mvua!

Kwahiyo unaporasmisha mali na kuwapa hati wakulima hawa ili wazitumie kupata mikopo benki na kwenda kuzarisha kwa kutumia mbinu wanayotumia hivi sasa bado unakuwa haujawasaidia sana, ni vyema ijulikane kuwa tatizo la msingi la wakulima siyo mitaji, bali ni kwa jinsi gani wakulima hawa wameandaliwa kuingia katika kilimo cha kisasa? Kama itakuwa ni kukopeshwa na kuendelea kuzarisha kwa mbinu za kijima itakuwa ni kuhatarisha mikopo, ni mapendekezo yangu kuwa ili mpango huu ufanyikiwe ni vyema uende samba mba na kuandaa wataalamu wa ugani ambao watafanya kazi ya kuhamasisha umma kuwa na fikra mpya za kuzarisha kitaalamu, tujiulize kwa hivi sasa ni vijiji vingapi vinao wataalumu wa kilimo.mifugo,uvuvi ambao hao ndio chachu ya kuleta mapinduzi katika uzarishaji?.

Si hivyo tu pia Mpango huu unapaswa uende sambamba na kuangalia ni kwa jinsi gani wataalamu hawa watawezeshwa kwa rasilimali mbali mbali ili waweze kufanyakazi zao kwa ufanisi mkubwa zaidi, kwa namna hiyo kweli tunaweza kuupunguza umasikini,Siyo lazima tunakiri mpango huu na kuuendesha kama ulivyo asisiwa na De Sato’’we should think globally but act locally “ kwani mazingira,utamaduni , mahitaji n.k yanatofautina baina ya bara na bara, nchi na nchi, mkoa kwa mkoa,wilaya kwa wilaya,tarafa kwa tarafa,kata kwa kata na kijiji kwa kijiji na kwa kuwa wanyoge walengwa wengi wako vijijini ni vyema tukajua hali halisi ilivyo na kuurekebisha mpango mzima ukaendana na mazingira yetu kwa kufanya hivyo tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi walio wengi badala ya kuwa na mipango mizuri katika karatasi tu.

Pili mfumo mzima wa masoko ya mazao ya wakulima lazima ueleweke na huwe wazi na wenye kuleta tija kwa wakulima, kwa hali ilivyo hivi sasa siyo soko huria bali ni shaghala baghala kwani wote tunaelewa katika soko huria kinachopanga bei ni’’ supply and demand’’ kinyume na ilivyo hivi sasa ambapo wafanyabiashara ukutana katika vikao visivyo rasmi na kupanga bei, mfano mwaka jana 2005 inasemekana wafanyabiashara wa korosho Lindi na Mtwara walikaa na kukubaliana kununua korosho kwa bei isiyozidi tsh 400/=kwa kilo jitihada za wakulima kususa kuuza hazijafanyikwa kwami hali imezidi kuwa mbaya sana kwani walanguzi hivi sasa wananua korosho hizo kwa bei isiyozidi tsh 200/=kwa mkulima hana la kufanya. Katika hali kama hiyo ata kama watakuwa wamepewa mikopo na kuzarisha bado tatizo la kurejesha mikopo litakuwa pale pale kwani mazao yao yananuliwa kwa bei ndogo kuliko gharama za uzarishaji.

Tatizo la soko ni kubwa mno siyo kwa mazao ya biashara tu bali ata mazao ya chakula na matunda, mfano hivi sasa mikoa ya kusini ni msimu wa maembe inasikitisha sana kuona maembe yanaharibika kwa kukosa soko la huakika,nenda Lushoto,Kabuku,Matombo,Iringa n.k hali ni hiyo hiyo.

Ni vyema ikaangaliwa ni kwa jinsi gani tatizo kama hili litatatuliwa kabla ya kwenda katika uzarishaji,swala la ‘’supply creats its own demand” halina nafasi kwa dunia ya leo.kwanini Shirika la viwanda vidogo vidogo lisiimarishwe(SIDO) ili liweze kutoa elimu ya ujasili amali ,masoko na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima bila hivyo mikopo haitasaidia kitu.

Vyama vya ushirika viimarishwe ili vilete ushindani katika soko pia viweze kuazisha viwanda vidogo na vikubwa vya kusindika mazao ya wakulima na kuyaongea thamani ,kwa kuendelea kuuza korosho ghafi,pamba n.k katika soko la ushindani ulimwenguni si tija kwa mkulima.

Tatu MKURABITA imeangalia tatizo la kutokupesheka kwa wanyonge wa Tanzania kuwa ni ukosefu wa hati ya kumiliki mali! Ambavyo si kweli kwani ni imani ya kibenki kuwa wateja wadogo wadogo hawakopesheki, na ni hatari(risk) kuwakopesha na ni gharama kubwa kuwahudumia na hivyo hakuna tija kwa benki na ikizingatiwa kuwa falsafa ya benki hizi za kigeni naza watu binafsi ni kutengeneza faida kadri inavyowezekana,kwani mwisho wa mwaka menejimenti itapimwa kwa kuangalia ni kiasi gani cha pesa zimepatikana kutokana na mtaji uliowekwazwa na wenye hisa(return on investment), ndio maana benki nyingi zipo tayari kuwekeza kwenye amana za serikali(Treasury bill/bond) pamoja na kujua kuwa faida inayopatikana kuwa ni kidogo lakini uwezekano wa kupata hasara ni mdogo(risk free investment) katika mazingira kama hayo hati tu haitoshi kukufanya ukopesheke, ni vyema zikawepo benki na taasisi za kiserikali ambazo zitatoa mikopo kwa wanyonge ambao benki za kigeni na za watu binafsi hazipo tayari kuwakopesha,

Nne ni vyema ikaeleweka nini maana ya dhamana katika biashara ya benki, kwa kawaida benki inapotoa mikopo ni lazima ijiridhishe kuwa pesa za mikopo zitarejeshwa na riba na iwapo ikatokea mkopaji akashindwa kurejesha mkopo kama ilivyotarajiwa basi dhamana uchukuliwa na benki na kuuzwa ili kufidia mkopo, kwa benki cha muhimu siyo thamani ya hati(paper value) bali ni kiasi gani kitapatikana kwa kuuza mali husika,ikizingatiwa kuwa siyo biashara ya benki kuuza mali(dhamana) ndio maana mara nyingi benki uteua chombo chenye utalaamu wa kufanya kazi hiyo mfano madalali wa mahakama n,k

Kwa kuzingata hilo benki inapofanya tathimini ya dhamana pamoja na mambo mengine uzingatia thamani ya mali katika soko (marketing value) na siyo thamani halisi ya mali (construction value) na ufanya hivyo kwa kuwa iwapo mteja atashindwa kutimiza masharti ya mkopo basi dhamana husika uuzwa na kitakocho hiakikishia benki kuwa dhamana ina thamani kiasi gani ni soko.


Pia benki inawajibika kujiridhisha kuwa mali hiyo ni rahisi kugeuzwa kuwa pesa katika soko kwani dhamana kama dhamana haitakuwa na maana yoyote kwa benki kami ni ngumu kuigeuza kuwa pesa(cash).


Ukiangalia mali za wanyonge wa Tanzania ambao asilimia 84 wanajishughulisha na kilimo na wanaishi huko vijivjini, na nilazima tuwe wa wazi na wakweli tunaposema wanyonge walioko vijijini tunamanisha hao,isije kutokea kuwa tunaondoa umaskini kwa watu wengine ambao mpango haukuwalenga,katika hali halisi hakuna benki itakayotoa mkopo kwa myonge mwenye hati ya shamba lililopo Ndapata au Kikulyungu huko Liwale mkoani Lindi au sehemu nyingine kama hizo kwani sehemu tajwa mashamba ni mapoli ambayo hayauzwi bali mwanakijiji anapohitaji shamba uenda kuomba katika serikali ya kijiji na kupewa, kwahiyo mkazi wa eneo kama hilo pamoja na kuwa na hati hawezi kupata mkopo toka benki yoyote,la sivyo tunaweza kukuta mpango huu unanufaisha baadhi ya mikoa na maeneo machache hapa nchini ambayo ardhi ina thamani,MKURABITA ni vyema ikanufaisha mikoa yote ya Tanzania,na hili iwe hivyo ni vyema maeneo yote yakaendelezwa kwa kuwekewa miundo mbinu ya kisasa na hivyo kuifanya ardhi kuwa na thamani(value),kinachoifanya ardhi ya Moshi,ArushamBukoba,Kilombero n.k iwe na thamani siyo hati. Viyo hivyo kwa nyumba zilizipo baadhi ya maeneo haziwezi kukubaliwa kutumika kama dhamana ya mkopo benki ata kama zina hati na gharama za ujenzi wa nyumba hizo ni mamilioni,thamani katika benki ni thamani iliyoko katika soko, kama nyumba haiwezi kuuzwa basi ni ‘’Valueless’’ kwa benki.

Mwisho ningependa kutoa angalizo/msisitizo. Ni vyema MKURABITA ukawalenga wanyonge wa Tanzania,nchi hii ni kubwa na viwango vya maendeleo na umaskini vinatofautiana sehemu moja na nyingine, kwa muda mrefu baadhi ya mipango ya serikali na wafadhili imeonekana kurundikana sehemu hizo hizo! MKURABITA isirudie makosa yale yale, mpango huu ulete uwiano wa maendeleo na upunguzaji wa umaskini nchi nzima isewa hadithi ya mwenye nacho ataongezewa au au maji utililika kutoka katika mito na vijito kuelekea baharini!ikiwepo dhamila ya dhati tunaweza kuufanya umaskini kuwa hitoria katika nchi hii, ni changamoto kwa rais wa awamu ya nne rais Jakaya Halfan Mrisho Kikwete 2005-2015.
MAKALA HII ILIWAHI KUTOKA KATIKA GAZETI LA TANZANIA DAIMA,IMEANDALIWA NA INNOCENT M.KAHWA,innokahwa@yahoo.com

Tanzania kila mtu analalamika!

Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Oxford toleo la pili,neno 'lalamika' linamaanisha kutoridhika na jambo fulani,au numg'unika.

Katika jamii,hutokea kuwa na watu ambao kulalamika ni silika yao.Watu wa aina hii ulalamika kwa kila jambo,kwao kila kitu hawaridhiki nacho.Hii ni tabia mbaya isiyo jenga.
Kulalamika si kubaya iwapo jambo linalolalamikiwa ni la msingi na anayelalamika kachukua hatua zote lakini kashindwa na hivyo ni muafaka kwa ngazi inayofuata.
Kulalamika tu hakusaidiii sana na hususan anayelalamika ikiwa ana uwezo wa kuondoa kero au tatizo na anaonekana hakuna jitihada zozote anazofanya ili kuepukana nalo na itokeapo kuwa ni kiongozi inakera sana.
Inavyoonekana, jamii ya Watanzania ni mabingwa wa kulia na kulalamika, na imefika hatua haijulikani nani analalamika na anamlalamikia nani na nani ni mtekelezaji,
Katika kuandika makala hii nimekumbuka hadithi niliyoadithiwa na rafiki yangu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa rais,wabunge na madiwani,kulikuwa na mtoto analia na ilipoulizwa kulikoni mtoto analia mama yake alijibu kuwa ni ccm, na alipoulizwa ccm wamefanya nini ,yule mama alijibu kuwa shida zote nchi hii zinaletwa na ccm.baadaye ilikuja kujulikana kuwa yule mtoto anatabia ya kuzurura hovyo na mama yake alikuwa amemzuia asiende kwa shangazi yake na hivyo abaki nyumbani,sasa zile lawama kwa ccm zinakujaje?
kila mtu anapenda kulalamika na kutotimiza wajibu wake.
Siku moja nikiwa likizo kijijini Bukoba, mzee mmoja alianza kulalamika kuwa fedha zao za kijiji zinaliwa,Mzee aliopoulizwa fedha zipi? Naye alijibu "tunazochanga" Alipoulizwa alikuwa amechanga sh ngapi,jibu lilikuwa yeye hakuchanga lakini wenzake walichanga!Hii ndiyo jamii ya Watanzania wepesi wa kulalamika pasipo kutimiza wajibu na kila mtu anafikiri mwenzake ndiye atatimiza wajibu.
Kwa kuwa viongozi ni zao la jamii, inaonekana nao wamekuwa ni viongozi wa kulalamika!Hivi majuzi nilishangaa kumwona Rita Mlaki naibu waziri wa Ardhi na Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokuwa nakagua ghorofa zinazodiwa kujengwa Masaki pasipokuwa naa kibali.
Kilichonishangaza ni kumsikia Naibu Waziri akilalamika akisema '' Huyu mtu lazima achukuliwe hatua na kama wizara itashindwa,basi suala hili itabidi alipeleke kwa Waziri Mkuu!"
Si hivyo hivyo tu amekaririwa huko mkoani Kilimanjaro baada ya kupokea malalamiko ya wananchi ambao walikuwa wanamlalamikia mwekezaji ambaye anaonekana kukiuka masharti ya shamba alilokkodishwa na wanaushirika, naibu Waziri aliahidi kulishughulia swala hilo haraka na kama atshindwa basi angelipeleka kwa rais!
Napata shida kumuelewa waziri anayeamua kushughulikia jambo wakati akiwa na dhana ya kushindwa kishwani mwake na kuwa mkombozi ni rais,kiongozi kama huyu anakuwa ameshindwa hata kabla hajaanza kutatua tatizo husika,ni vyema viongozi wakajenga dhana ya ushindi vichwani mwao.
Kutojiamini ni ugojwa ambao haujenge uthubutu,hifanya jamii kuganda na hivyo kuwa kikwazo kwa maendeleo.Inakuwa mbaya ugonjwa wa namna hiyo unapokuwa umewashika viongozi wetu.
Miaka ya nyuma niliwahi kusoma katika gazeti moja hapa nchini,mahojiano ya ya aliyekuwa katibu mkuu wa rais awamu ya kwanza ndugu Timoth Apiyo akilalamika kuwa pensheni anayopata haitoshi kabisa,hivyo anaishi kwa taabu.Kilichinishangaza si kwamba pensheni haitoshi,bali ni kujiuliza, je, ni kwa wakati gani pensheni imeonekana haitoshi?
Kiongozi huyu alikuwa na nafasi kubwa ya kuweza kubadilisha maisha ya wastaafu lakini akiwa madarakani hakuliona hilo,kama yeye alishindwa kufanya mabadiliko anatarajia nani atekeleze hayo?
Juzi pia Naibu Waziri wa Fedha ndugu Mustapha Mkulo amekaririwa na vyombo vya habari akizitaka taasisi zinazojihusisha na mafao ya uzeeni ,kwani hayaendani na wakati, Mkulo kabla ya kustaafu alikuwa mkurugenzi mkuu wa NSSF na alikuwa na nafasi nzuri kufanya hayo anayoyapendekeza hivi leo.Swali la kujiuliza ni kuwa ,je, hivi baada ya kustaafu ndipo alipogundua kuwa mafao ya uzeeni hayatoshi?
Tunatakiwa kuwa na viongozi wenye visheni,wanaoona mbali, wasioangalia maslahi binafsi kwanza kabla ya kuangalia ya wengine ,kwa sababu hayo wanayoyaona yamekuwepo na yamekuwa yakilalamikiwa na wadau kwa muda mrefu.
Naye Waziri wa Usalama wa Raia,Harith Bakari Mwapachu,alikaririwa na vyombo vya habari akilalamika msongamano wa mahabusu na kuahidi kuwa itabidi awasiliane na waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba ili kuzipitia na kuzirekebisha sheria na taratibu .
Swali la kujiuliza; je,yeye alivyokuwa Waziri wa Sheria na Katiba kwa miaka 10 chini ya awamu ya tatu,tatizo hili hakuliona? Mbona malalamiko na mapendekezo hayo yamekuwepo kwa kipindi kirefu hko nyuma! Hivi ndivyo viongozi wetu walivyo.
Orodha ya viongozi walalamishi ni ndefu,Mbunge wa Igagula,Tatu Ntimizi,amekaririwa akisema kuwa ingawa amestaafu upoli miaka kadha iliyopita,hajapata marurupu yake,kwa madai kuwa hakufaulu somo la Kiswahili kigumu wakati alipokuwa mtumishi katika Jeshi la polisi .
Ntimizi alikuwa naibu Waziri katika awamu ya Tatu, kwa muda mrefu aliokuwa naibu waziri alijua fika kuwa baadhi ya kada za watumishi serikalini hutahiniwa katika somo hilo na watumishi wengi wamekuwa wakilalamika juu ya utaratibu huo.
Swali la kujiuliza ni kwamba alipokuwa naibu waziri alifanya jitihada gani kurekebisha utaratibu huo? au ndiyo mwenye shibe hamjui mwenye njaa?
Naye Mbunge wa jimbo la Kisarawe mkoani Pwani ,Athuman Janguo,hakuwa nyuma ,amekaririwa na nyombo vya habari nyuma akisema kuwa ingawa aliwahi kuwa katibu mkuu wa wizara,alipokwenda kufuatilia pensheni,vijana wa Idara ya pensheni walimtaka aonyeshe barua ya uteuzi kuthibitisha kuwa aliwahi kushika madaraka hayo makubwa.
Janguo anasahau kuwa utaratibu huo umekuwepo muda mrefu na haukuanzishwa hivi leo.alipokuwa katibu mkuu wangapi walikwamishwa na yeye akiwataka kutimiza utaratibu huo,
Janguo aelewe kuwa tatizo si vijana aliowakuta pale Idara ya Pensheni,tatizo ni sheria na taratibu walizoziacha wao.Laiti wangezibadilisha enzi zao wasingezikuta,na ni vyema aelewe kuwa sheria zikifuatwa vizuri hazibagui kuwa huyu alikuwa katibu mkuu,mkurugenzi,karani au mhudumu.
Uhuru wa vyombo vya habari na mageuzi katika sekta ya mawasiliano ,vimesaidia sana kuwaelewa viongozi wao,lakini nichokuwa na uhakika nacho ni; je, viongozi nao wanawaelewa wananchi wao?
Ni maoni yangu kuwa viongozi wasituaminishe kuwa rais wetu ni wa miujiza,kwamba ni rais anayejua yote na kuweza yote na hivyo ni lazima kila kitu kipelekwe kwake, kuna mambo yanaweza kushughulikiwa na kutekelezwa na mtu binafsi,kiongozi wa kitongoji,kijiji,kata,tarafa,wilaya.mkoa,wizara,taasisi,sekta,idara n.k hakuna sababu kwa kila kitu kukimbiza kwa rais.
Mwezi uliopita ,nilishangaa na kustuka niliposoma kichwa cha habari cha gazeti moja kikisema wabunge kumuona Rais Kikwete ili asaidie makandarasi wazerndo,
Habari yenyewe ilieleza kuwa,Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Miundombino ya Bunge,Getrude Mongelle,ameshauri waonane haraka na Rais Kikwete ili aweke msukumo wa makusudi utakaosaidia kuwainua makandarasi wazarendo.Alisema haikubaliki kuona kampuni za kigeni zinakamata asilimia 80 mpaka 90 za ukandarasi nchini .
Kilichonishangaza si kilio cha wabunge,la hasha,kwani natambua umuhimu kiuchumi kama kazi hizo zingefanywa na wakandarasi wazarendo pesa hiyo ingebaki hapa nchini na faida nyingine nyingi ambazo si madhumuni ya makala hii hivi leo.
Najiuliza,hivi kutunga sheria na taratibu za kuwezesha kuwainua makandarasi wazarendo kunahitajika nguvu ya rais? Je, viongozi waliopewa dhamana na madaraka ya kusimamia hawalioni hlio?
Nakama rais analiona kuwa ni tatizo lakini viongozi wanaowajibika kulishughulikia hawawezi mpaka wapate msukumo wa rais,basi hapo kuna tatizo.Aidha litakuwa siyo tatizo hata kama rais atakuwa ameshinikiza litekelezwe,au viongozi hao hawapaswi kushika dhamana hizo walizo nazo,tunatakiwa kuongea lugha moja katika kushughulika matatizo ya yetu, na kila mmoja atimize wajibu wake na Tanzania yenye neema itawezekana,
Makala hii imetoka katika gazeti la Tanzania daima la 13 April 2006, ambapo uwa naandika makala mbali mbali ,imeandaliwa na Innocent M.Kahwa,innokahwa@yahoo.com