Sunday, April 16, 2006

KAMPENI NI NJIA YA KUWASILIANA NA WAPIGA KURA

Kwa takribani yapata miezi mitatu tangu kampeni za uchaguzi wa madiwani,ubunge na urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania zianze na hatima yake ni mwezi huu tarehe14 ambayo ni siku ya kupiga kura.

Kimsingi wanasiasa kipindi chote hicho wamekuwa katika soko tena soko huria wakijaribu kunadi sera, katika soko kinachonadiwa ni bidhaa(product) yaani kitu chochote kinachoweza kutolewa na kuridhisha hitaji la mtu, na ieleweke kuwa katika kampeni kinachokuwa kinauzwa ni sera na mzarishaji(producer/manufacturer) ni vyama, na tukiangalia katika soko letu hili kulikuwa na wazarishaji mbali mbali kuanzia wadogo mpaka wakubwa, kama ilivyo katika biashara za kawaida ambapo kuna makampuni makubwa mfano katka soko la vinywaji baridi kuna kampuni inauza coca cola,pepsi cola,super cola n.k vivyo hivyo katika soko la siasa kulikuwa na vyama kadha wakadha kama vile CCM,CUF,CHADEMA,TLP,NCCR-mageuzi,CHAUSTA,UDP n.k

Ukubwa wa kampuni yeyote unategemea na vigezo unavyotumia, unaweza kutumia asilimia ya umilikaji wa soko(%market share),mauzo(sales) n.k sawia katika ukubwa wa chama unaweza kuangaliwa kwa kutumia vigezo tofauti kama vile idadi ya wanachama,idadi ya wabunge na madiwani,mtandao wa chama, idadi ya washabeki na wapenzi n.k

Katika soko la bidhaa za kawaida kama vile soda,magari,simu,hotel,benki,muziki n.k umuhimu mkubwa hawekwi kwenye bidhaa(product) bali uzingatiaji mkubwa uwekwa kwa mtumiaji/mnunuzi(consumer/customer),afisa masoko mzuri ataweka kipaumbele zaidi katika hitaji la mteja kuliko bidhaa, kwani bidhaa utumika kama behewa(vehicle) la kutatua shida ya mteja.Hivyo ni vyema na busara sana ukajua mteja anataka nini? alafu ndiyo ukatengeneza bidhaa ya kuweza kutatua tatizo lake, vivyo ilivyo katika siasa ni vyema chama kikaanza kujiuliza mwananchi anashida gani? Kutokana na shida au tatizo husika ndipo sera uandaliwa kukidhi shida inayomkabili mwananchi, chama kisicho zingatia hayo kitegemee muujiza zaidi kupata kura za mwananchi labda katika soko la walaji wasiojua wanataka nini?.

Haitoshi tu kuwa na bidhaa nzuri kiwandani au dukani pasipo kuwasiliana na wateja au walaji(communicate the value to customers) ndiyo maana vyama vyote vya siasa baada ya kuwa vimejua shida na kero za wananchi vilikaa chini na kuandaa sera zenye kutoa majibu ya matatizo ya wananchi , sera kama vile za elimu,afya, kilimo,ufugaji,madini ,maji, ajira n.k chama chochote kitakuwa kimefanya kosa kubwa sana kwa kuandaa sera na kukaa nazo tu ofisini pasipo kuwasiliana na wananchi.

Katika siasa za ushindani kuna njia nyingi zinazoweza kutumika kujitangaza, lakini kabla hujaamua ni njia ipi itumike ni vyema mambo yafuatayo yakazingatiwa

Kwanza adhila iliyokusudiwa, akina nani? ni vijana, wazee,wanawake, wanaume,wakulima, wafanyakazi,wavuvi n.k ni muhimu sana kuijua adhila katika kampeni mara nyingi wapiga kura katika nchi maskini ni vijana na watu wa rika ya kati na wanawake, wazee sana ni wachache pamoja na hayo haipaswi wazee kudharauliwa na kuachwa maana katika uchaguzi kura moja ina thamani kubwa katika kuamua mshindi, mgombea aliyefanyikiwa kujua adhila anayowasiliana nayo anakuwa na nafasi kubwa sana kufikisha ujumbe uliokusudiwa, katika mawasiliano kuna hatua zifuatazo kwanza mtumaji (sender) pili ujumbe(massege) tatu njia(means) na nne mpokeaji(receiver) na mwisho ni mshindo nyuma (feedback) ni vyema ujumbe ukafika na ukaelewaka la sivyo itakuwa ni kazi bure na ndiyo maana baadhi ya wagombea baada ya kugundua kuwa adhila ni vijana wasikuwa na kazi lugha au maneno kama haya yalisikika yakutumika’’ washikaji’’ ,‘’mmepigika’’, ‘’hakuna kulala mpaka kieleweke’’ nk hii yote ni njia ya kutengeneza ujumbe utakao eleweka na adhila husika.

Si hivyo tu, bali habari gani wanataka ? ni vyema mgombea akajua kuwa pamoja na kuwa kila chama kina ilani ambayo ni mjumuisho wa sera zote kwa ujumla wake adhila yake inataka kusikia nini? kwa mfano mgombea anayewasiliana na wapiga kura walioko machimboni Mwadui,Geita,Melelani n.wangependa sna kusikia zaidi sera inayohusu madini ,itakuwa ni kupoteza muda na fedha bure kuwaeleza habari za uvuvi au kilimo n.k.

Chombo gani kitumike? Mgombea ni vizuri akajua wapiga kura wake wanapendelea zaidi chombo gani cha mawasilino kama ni Radio na mgombea yupo Dar es salaam ni vyema akafikiria Radio za FM na pia ni lazima ajue ni fm gani? Kama ni tv ni tv gani ? kama gazeti ni gazeti gani? n.k

Pili mgombea sharti akajua lengo na dhumuni la kuwasilina ni nini? je ni kujitambulisha( creating awareness) ,kushawishi (convince), kukubusha(remind) au ni vyote kwa pamoja maana katika kampeni mgombea anaweza akawa ndiyo kwanza anajitambulisha pia akawa anajaribu kushawishi ili yeye aonekane ndiye bora na hivyo achaguliwe yeye pia inaweza ikiwa anawakumbushia tu kuwa yeye ndiye mgombea bora, katika mazingira ya namna hioyo ni vyema mgombea akaonyesha ni kwanini achaguliwe yeye na si mshindani wake na hivyo haiepukiki kutomuongelea mshindani wako ili yeye aonekani hafai akilinganishwa na wewe, na wewe ndiye unafaa kuwa diwani,mbunge au rais hapa swala siyo kukashifiana na kuzushiana mambo ya ovyo bali kuongelea sifa zako za msingi ukizilinganisha na za mshindani wako,ni vyema mgombea akajenga uhaminifu(loyalty) kwa wapiga kura ili ata akija mshindani wake haseweze kuwageuza wapiga kura wake na hivyo siku ya kupiga kura tarehe 14 mwezi huu wampigie yeye, ukiwa na wapiga kura "wasiyokuwaroyal" kwako basi ujue bado haujafanyikiwa kuwanasa.

Tatu katika kampeni kuna njia nyingi za kuweza kuwasilina na wapiga kura yaweza kuwa ni tangazo katika gazeti ,radio,tv ambapo ujumbe fulani mfano ‘’…kwa maendeleo ya taifa lako mchague x’’ pia mahusiano(publicity and public relations) ni muhimu sana kwa chama na mgombea yeyote aliyedhamiria kushinda katika uchaguzi wa tarehe14 mwezi huu, njia hii utumika kujega na kuimarisha jina zuri la chama au mgombea na kuzika habari mbaya za chama au mgombea mfano endapo itatokea chama Y kikahusishwa na habari mbaya ni vyema juhudi zikafanyika kujenga jina zuri la chama au mgomnbea katika kipindi hiki cha uchaguzi vyama na wagombea mbali mbali vimeonekana kufanya hivyo katika kipindi hiki cha uchaguzi na ni jambo zuri na kupongezwa kwani inaonyesha ni kwa jisi gani walivyo makini na kuendesha mambo kitaalamu. Pia mabango,kofia,t-shirt,khanga,vipeperushi hizo zote ni njia za kujitangaza kwa wapiga kura na ni kweli kuwa vitu hivyo vinahitaji pesa nyingi sana na hivyo ni vyema vyama vikawa vinajiandaa kwa hilo, uchaguzi hapa Tanzania ufanyika kila baada ya miaka mitano ni muda wa kutosha kwa chama makini kuweza kuwa na mpango wa kutenga bajeti kidogo kidogo kila mwaka na inapofika mwaka wa uchaguzi tayari chama kinakuwa na pesa kwa ajili hiyo, tatizo lililopo kwa vyama vingi ni kuendesha mambo kwa mpango wa zima moto,uchaguzi siyo jambo la kushutukizwa ni jambo linalo julikana kabla ya miaka mitano,

Vyama kukaa na kulalamika kuwa havina fedha za kampeni si la msingi sana bali jitihada zifanyike mapema kutafuta pesa na wakati mwingine ni swala la uvivu wa kufikiri na kutokuwa wabunifu tu, ni nani aliyejua au kutarajia kuwa chama fulani kingiweza kutumia helikoputa, kwa mwaka huu helikoputa inachukua nafasi zaidi ya usafiri ni ‘’promotional material’’inamtangaza mgombea na chama husika ina kijenga chama kwa wapiga kura huu ni ubunifu wa chama badala ya kutumia vitu ambavyo ni ‘’traditional’’ chama kinakuja na kitu kipya kwa mazingira ya uchaguzi wa Tanzania na 2010 helikoputa inaweza isiwe kivutio kama mwaka huu hiyo ndiyo chamgamoto ya kusoma wakati na mazingira na kuyatawala. Mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine.

Kama ilivyo biashara huria ilivyo jaa ushindani mkubwa sana vivyo hivyo siasa ya vyama vingi ina ushindani mkubwa sana, zama za kukaa maofisini na kuandaa sera pasipokujua ni nini matatizo ya wananchi zimekwisha,zama zakuleta wagombea bila kujali wapiga kura wanataka kiongozi wa aina gani ili waweze kushirikiana naye kuleta maendeleo hazipo tena,wakati wa bidhaa mbovu na hafifu sokoni haupo tena wakati wa sasa ni wa mzarishaji kwanza kujua hitaji la mteja na kutengeneza bidhaa inayokidhi hitaji na kuwasiliana na mteja ukimjulisha kuwa bidhaa safi na bora iko sokoni.

Wakati umebadilika na unazidi kubalika tena kwa kasi ya ajabu sana siasa ya leo si ya jana na siasa ya kesho si ya leo,inahitajika viongozi wasiyosubiri mabadiliko yawabadilishe wao bali viongozi wanaoleta mabadiloko na kuyasimamia mabadiliko hayo,

Mengi yamesemwa, mengi yameandikwa,ahadi nyingi zimetolewa , kilikuwa ni kipindi cha wagombea na vyama vyao kusema na kusikilizwa sasa ni zamu ya wapiga kura kusema kuwa tumewasikia na kuwaelewa na hiyo itafanyika kupita kura yako wewe mwanachi uliyejiandikisha , ni wakati wako kusema kilicho ndani ya mwoyo wako na wala usishinikizwe na ahadi ya uhongo,takrima,rushwa,ukabila,udini we sema tu siku hiyo ya tarehe14 mwezi huu na tume ya taifa ya uchaguzi itatangaza kwa sauti kubwa nini ulichokisema kwa kweka alama ya NDIYO kwa chaguo lako la diwani,mbunge na rais

Makala hii ilitoka katika gazeti la Tanzania daima mwaka jana kabla ya Uchaguzi MkuuMUANDISHI NI MSOMAJI NA MMFUATILIAJE WA SIASA ZA NDANI NA NJE YA TANZANIA

MWISHO

11 Comments:

Blogger Ndesanjo Macha said...

Ndio Inno,
Karibu sana. Ni furaha kubwa kuona tumepata mwanakijiji mpya katika kijiji chetu cha blogu.

Ningependa kujua kwa undani zaidi tofauti ulizo nazo nami kimtazamo!

Halafu unaweza kutumia Ripway: http://www.ripway.com
kuhifadhi makala zako.

8:12 AM  
Blogger Jeff Msangi said...

Inno,
Karibu sana.Ni wazi kabisa kwamba mchango wako ni muhimu katika ulimwengu huu wa habari na mawasiliano.

11:19 AM  
Blogger boniphace said...

karibu Ino sasa hapo kazi kwenu kupambana na Mwananchi maana huko kila mtu anamiliki sasa Gazeti Tando. Karibu sana

3:41 PM  
Blogger mwandani said...

Karibu. na ahsante kwa kuainisha masuala ya kampeni za siasa. safari bado ndefu.

9:50 PM  
Blogger innocent said...

Ahsante sana kwa kunifumbua macho jinsi ya kutumia blogu,nitaboresha kadri nitakavyo pata ujuzi, nimekuwa nikisoma makala zako kwa muda mrefu hususan ulipokuwa unaandika katika gazeti la Rai, kuna baadhi ya makala zako zinakuwa za nadharia sana na hazitekelezeki ,kwa kuwa sikuwa nimejiandaa kuelezea hilo,nitatoa mfano ninaoukumbuka miaka ya nyuma uliandika kuhusu waafrika tulikuwa na dini zetu nzuri na majina yetu mazuri lakini tumeyaacha na ulihimiza kwamba tusiwe watumwa tuendelee kuzifuata,hapo sikubaliani nawe,nitakuandikia kwa kirefu siku nyingine,

1:04 AM  
Blogger Ndesanjo Macha said...

Innocent,
Asante. Kuna faida kubwa ya kukutana na mawazo tofauti na yako. Hii inasaidia sana kwani changamoto ya kimawazo inasaidia kumkuza mtu na kumuimarisha. Nitafurahi sana kupata undani wa mawazo yako yanayopingana na mitazamo yangu. Tuna ukumbi mzuri wa kujadili mambo haya, yaani blogu zetu.

6:09 AM  
Blogger Rama Msangi said...

Karibu sana mpiganaji. Safari yetu ni ndefu sana kufika tuendako lakini tukiwa wengi inakuwa rahisi sana maana hata maongezi na vicheko hupunguza urefu wa safari.

6:31 AM  
Blogger Innocent Kasyate said...

Karibu wajina wangu.Mambo ni kutandaa tu.

8:18 AM  
Blogger imanauliya said...

I like it this really good information
Vimax asli
Vimax pills
Obat perangsang wanita
Boneka Full Body
Obat Vimax
Meizitang Botanical

10:44 AM  
Blogger zarena cantik said...

perfect perfect fried rice, good post for the beginners as well..Super Prema, loved the presentation very much
Selaput Dara Buatan
Vimax asli Canada
Obat Perangsang
viagra usa
Bio Slim Herbal
Obat Mata Herbal
Perangsang Wanita
Obat Perangsang Cair
Perangsang Sex Drops
Vimax Oil
Semenax
Vagina Tabung
Vagina Center
Boneka Full Body
Vagina Pinggul
Alat Bantu Sex Pria
Vagina Elektrik
Penis Elektrik
Penis Tempel
Penis Manual
Penggeli Vagina
Penggemuk Badan
vimax canada

5:52 PM  
Blogger Unknown said...

VIMAX ASLI
ALAT SEX UNTUK PRIA
VAGINA PANTAT NUNGGING
VAGINA TABUNG
VAGINA SENTER
BONEKA FULL BODY
ALAT SEX UNTUK WANITA
VIBRATOR LIDAH
PENIS TEMPEL GETAR ELEKTRIK
PENIS SILIKON GETAR
PENIS IKAT PINGGANG
BONEKA FULL BODY PRIA
PENIS MUTIARA
VIBRATOR PENGGELI
ALAT PEMBESAR PENIS
VAKUM PEMBESAR PENIS
PRO EXTENDER
ALAT PEMBESAR PAYUDARA
VAKUM PAYUDARA
KRIM PAYUDARA
dr SUSAN CREAM
KONDOM
KONDOM KRISTAL
KONDOM NAGA
KONDOM KAKTUS
MINYAK PEMBESAR PENIS
COBRA OIL
BLACK MAMBA OIL
LINTAH PAPUA
OBAT KANTUNG MATA
OBAT PENGHILANG KANTUNG MATA
OBAT KUAT SEX
KAMAGRA OBAT KUAT CAIR
OBAT KUAT SEMPROT PROCOMIL SPRAY

9:24 AM  

Post a Comment

<< Home